Nawezaje kuiokoa familia yangu na mateso ya jini huyu?

Nyie ni Waislam? Tuanzie hapa kwanza.
 

Kusoma Ilipoanzia

Sehemu ya Pili

-----

"NITAFUPISHA HAPA, IKUMBUKWE HII NI STORI YA MAISHA YANGU KABISA KWA MUDA WA MIAKA 7, NIMEKUA NIKUZUNGUKA HUKU NA KULE KUTAFUTA MSAADA KWA KIPINDI HIKO CHOTE. NILITAMANI KUELEZEA KILA STAGE NILIYOPITIA ILI MWENYE UWEZO WAKUSAIDIA MAWAZO AJUE NIWAPI ANAWEZA SAIDIA."

J3 Tumeamka nimeendelea na kazi za kila siku, Ila hapa kuna maisha kidogo yalikua tofauti, Wife alikua ananiambia vitu vingi na vinatokea, Mala nyingi akisema jambo na likatokea, Mfano nakumbuka alishanifanyia matukio mawili ndani ya siku 1, Siku hiyo alikua na mimba ya miezi kama minne nmetoka nampeleka pharmacy akanambia tu kiutani anatamani kuokota hela.

Basi nikawa namcheka tu nikapuuzia, tulipo kua tukirejea toka Pharmacy akanambia kachoka hawezi tembea nikaita Tax, wakati nakaribia kwenye Tax alinionyesha kibunda Kikiwa chini usawa mlango wa gari, akakiokota ilikua ni laki8, nilipata mshangao akacheka alafu hakusema kitu.

Tulipofika home alikuja rafiki yake kumuona, banda ya stori kadhaa akamwambia, leo atakama unaharaka vipi usipande bodaboda, akapuuzia alipokua akiondoka akadai kachelewa akaita boda, azikupita dakika 10 tunapigiwa simu wamedondoka kaumia vibaya.

Akawa ni mtu wa aina hiyo lakini lile tatzo lakukabwa halikuisha, Shida nyingine ikaja ata nikitongoza demu popote atajua hiyo kitu nayo imekua ikinivuruga sana.

Kuna sheikh mmoja yupo Ilala anaitwa sheikh Khalfan sikumoja baada ya dua alinambia tatzo la huyu jini wa mkeo ukisema uingize pesa yako kumtibu mkeo anakufungia kila kitu utaishiwa utakosa mpaka hela ya maji ya kunywa,

Na nikweli nakumbuka nimesha mpeleka wife kwingi nikifanya kutafuta tiba, basi nitapoteza kilakitu, yaani taishiwa na kazi tapoteza kabisa, Sasa ndugu zangu inawezekanaje kumuacha mwenzio akiugua kwa kuhofia hayo, Tatzo la hii michezo sio kama anakua kichaa au vipi hapana.

Ili niishiwe pesa tu naweza pata series ya wagonjwa, ndani ya mwezi mzima akaugua yeye, akaugua mama nyumbani wakawa wapokezana, ni mwendo wa hospital tu, imekua hivyo kwa muda sana.

.. Naomba niishie hapa kwa sasa, kwa mwenye uwezo au kujua wapi naweza pata njia ya kweli ya kutatua hili karibuni.
 
Wewe toka mwanzo kwa nini ulishindwa kuijulisha familia yake
 
Ukitulia tu, mwisho wako hautakuwa mzuri kama utaendelea kuishi na huyo mkeo.
Mpeleke kwenye maombi;- jaribu kwenda arusha umpeleke ngurumo ya upako, kwa sababu kuna wengine hutoka nje ya nchi na kwenda pale kwa msaada.
 
Huko kwa waganga na mashekhe uchwara ndo umeenda kumuongezea madudu zaidi,kwasie wakristo huyo kabla hajafunguliwa anatakiwa afanye toba ya maagano aliyojiunga nayo ama yaukoo wao,then afanyiwe deliverence hicho kidude kitapigwa moto mpaka na aliyekituma wote watasambalatika . NB: Matatizo mnayataka wenyewe kwakupenda kwenda kwa waganga mnaacha kumtafuta Mungu mwenye nguvu kuliko hao waganga mashetani
 
Nakazia hapa, wiki hii kuna maombi ya staili hii hapo K.K.K.T Kimara Korogwe kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa mbili na nusu ni kila siku yataendelea hadi wiki ijayo hadi pasaka ukipata mda njoo nae hutajutia wala hutatumia hata senti.
 
Pole sana mkuu, kweli dunia ina mambo kama wasemavyo watu pori.
Najua wataalamu wa miziziology na tiba mbadara watakuja kukupa mwongozo.
 
Hakuna pepo awezae mtoa pepo wote ni kampuni moja awatupani, zaidi utapewa jini Mkubwa amtulize jini Mdogo baada ya mda itarejea tena hali.
Hakuna ushirika Kati ya mwanadamu na majini, Kazi ya jini ni kuuwa.
Ukiyakataa na kuyafurusha yasitawale maisha yako utakuwa salama.
 
Why mnarudi nyumba hiyo hiyo
Hebu Hama nyumba uone
Shida ni binti na sio nyumba.
Binti aliweka maagano au kwao binti anatoka ukoo wa kichawi,kiganga,kitemi au kichief ni rahisi kufatiliwa na roho wa chafu.
Mfano ugonjwa wa sicocell,kifafa chanzo ni uzao ukoo wa kichawi au uganga au wa kimaagano ya kichawi.
Kama nyumba ndo Ina vitimbi basi hio nyumba imejengwa juu ya madhabau ya kichawi,au zamani eneo hilo ilikuwa ni kilinge cha mganga au ilikuwa ni eneo la matambiko au ni lango la kuzimu au mmiliki wa nyumba hio ni agent wa kuzimu au ni member wa freemason ikiwemo nyumba hio imejengwa kwa pesa za shetani.
 
Naitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.
Mh. Mkimbilie Mungu ndio msaada sio waganga
 
Aisee! Pole sana mwamba.
 
Tunahakikishaje haya mambo yametokea kweli na.

1. Si hadithi ya mtu ya kutungwa tu.
2. Si matatizo ya akili ya mtu yanayotafsiriwa kama uchawi. Maana tushaambiwa Tanzania kuna watu wengi wana magonjwa ya akili hayajanyumbulishwa. Sasa tunajuaje haya nayo hayaingii humo?

Isije kuwa mtu ana kifafa cha aina yake hakijulikani vizuri, anaona double double mapicha ya kutisha, anajidhuru mwenyewe bila kujua, tunasema uchawi.
 
Wew jamaa cjajua ni dini gani ila naona tu hapo visomo na mashehe.. sasa basi nakushauri tafuta huu mwamba wa uzima YESU KRISTO hakuna tatizo lililoshindikana hapo upate tu sehemu sahihi..kua na imani..hakuna jina lingine chini ya mbingu wala popote liwezalo kuokoa zaidi yake..
 
unajua najiuliza mtu mpaka anapitia wakat mgumu kama huu na haon sululisho wakat ni jambo dgo sana hili, najiuliza ni kuwa spidi ya Yesu kutanganzwa duniani imepungua au watu wenye matatizo kama yako wanasikia lakini wanapuuza...?
.
nimegundua kuwa Yesu yupo kila mahali zaid ya robo tatu ya coment wamekwambia uende kwa Yesu na nauwakika mtaani ndio zaidi huwa unasikia habari za Yesu kuokoa watu.
.
Yesu alisema atakayekuikoa nafsi yake mwenyewe ataipoteza bali aipotezae nafsi yake kwa yeye(Yesu) ataokolewa.
.
uchaguzi ni wako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…