Nawezaje kuishi bila kazi yeyote, tusaidiane

Marry Diana

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2025
Posts
1,429
Reaction score
4,125
Shikamoon wakubwa

Mwishoni mwa mwaka Jana niliweka mipango yangu kuwa ifikapo tarehe 5 Mwezi wa Kwanza niwe nimeshalipa chumba changu,ikiwa ni njia ya kujitegemea, wazazi wangu ,haswa mama hakupenda kabisa nihame nyumbani huku akiniasa ikiwa maisha ni magumu nirudi.

Mmmh ,nikalipa chumba miez mi3 maeneo ya jirani na nyumbani,
Huku nikijipanga namna nyingine,

Kilichonikwamisha ni vibarua vya hapa na pale,wengi ni wanalipa miezi miwili ya mwanzo kunakoelekea ni Kesho keshokutwa kitu ambacho sikupenda.

Sasa nahitaji mnipe aidia ya biashara ,mama kasema atanipa kiasi kisichopungua milion moja na nusu nikijiongeza naweza tengeneza kitu ,

Jamani Mimi sijiuz,sihitaji bwana wala Nani ,komenti yako iwe inahusu maisha.

Asanteni
 
Wewe unapendelea kufanya kitu gani?

Wazo la kupewa ni zuri lakini ikiwa sio kitu unachopenda hakitafika mbali!
Ungeweka mawazo yako, mapendekezo yako watu wakushauri kupitia uzoefu wao.
 
Shikamoon wakubwa

Mwishoni mwa mwaka Jana niliweka mipango yangu kuwa ifikapo tarehe 5 Mwezi wa Kwanza niwe nimeshalipa chumba changu,ikiwa ni njia ya kujitegemea, wazazi wangu ,haswa mama hakupenda kabisa nihame nyumbani huku akiniasa ikiwa maisha ni magumu nirudi.

Mmmh ,nikalipa chumba miez mi3 maeneo ya jirani na nyumbani,
Huku nikijipanga namna nyingine,

Kilichonikwamisha ni vibarua vya hapa na pale,wengi ni wanalipa miezi miwili ya mwanzo kunakoelekea ni Kesho keshokutwa kitu ambacho sikupenda.

Sasa nahitaji mnipe aidia ya biashara ,mama kasema atanipa kiasi kisichopungua milion moja na nusu nikijiongeza naweza tengeneza kitu ,

Jamani Mimi sijiuz,sihitaji bwana wala Nani ,komenti yako iwe inahusu maisha.

Asanteni
Anza kwa kuuza vitu vya kike kwa kutembeza,kwa wanawake wenzio
 
Kama upo nje ya mkoa ambao mazao ya ziwani ni magumu kupatkna, basi hyo millioni moja ni hela nzuri kuanza biashara za dagaa, hususani uwe unatoa kule mwanza unapeleka unakodhani ni pazuri
-dagaa za mwanza hazijawahi kukataa popote
 
Back
Top Bottom