Shikamoon wakubwa
Mwishoni mwa mwaka Jana niliweka mipango yangu kuwa ifikapo tarehe 5 Mwezi wa Kwanza niwe nimeshalipa chumba changu,ikiwa ni njia ya kujitegemea, wazazi wangu ,haswa mama hakupenda kabisa nihame nyumbani huku akiniasa ikiwa maisha ni magumu nirudi.
Mmmh ,nikalipa chumba miez mi3 maeneo ya jirani na nyumbani,
Huku nikijipanga namna nyingine,
Kilichonikwamisha ni vibarua vya hapa na pale,wengi ni wanalipa miezi miwili ya mwanzo kunakoelekea ni Kesho keshokutwa kitu ambacho sikupenda.
Sasa nahitaji mnipe aidia ya biashara ,mama kasema atanipa kiasi kisichopungua milion moja na nusu nikijiongeza naweza tengeneza kitu ,
Jamani Mimi sijiuz,sihitaji bwana wala Nani ,komenti yako iwe inahusu maisha.
Asanten