Hii ya dagaa kama utahitaji kufanya, fanya hivi, nunua wale dagaa wa mafuta PURE namaanisha wale waliokaangwa wakiwa wabichi kabisa, then funga kwenye package kadiri utaona inafaa, zunguka mashuleni, supermarket peleka mzigo, lakini pia tafuta connection na manesi mahospitalini ndio mboga zao hizo, ukitumia laki 3 Kwa kuchukua mzigo lazima upate faida ya 50 Hadi elfu 70, hivyo upatikanaji wa dagaa na namna utaagiza mara nyingi ndivyo utapata faida nyingi/kubwa Kwa mwezi, ukihitaji mtu wa kukutengenezea dagaa nzuri inayojiuza sokoni niambie nitakuunganisha
Yeye huyu mtu anachofanya ni anaenda asubui kukununulia dagaa Kwa wenye mitumbwi, then anakukaangia, halafu akimaliza anapiga hesabu zotee zilizotumika kuanzia kununua Hadi kukaanga then unalipia anakutumia mzigo wako
Nimechoka ku type, ila najua mengi kuhusu hii biashara maana ninaifanya, ukihitaji kuuliza chochote karibu uliza hapa hapa nitakujibu
NB: Ukipata wateja wa hii kitu hutokuja kuwaza stress ya pesa,