Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Habari wakuu

Nimehangaika sana kukabiliana na hili jambo lakini kwa uwezo wangu wote imeshindikana kabisa nahitaji msaada na ushauri haswa wa kiimani

Lakini msaada huu sipendelei munielekeze kwa manabii wala mitume wala dini nyingine tofauti na ukristo
Kama una mchungaji unamfahamu ambae ana uwezo wa kuongea na Mungu direct na shidq yangu ikatatuliwa naomba mni comments hapA

Tatizo linalonisumbua ni hili

Mimi ni binti wa umri wa miaka 26.. mwaka fulani nilipata mchumba wa kutaka kunioa.. wakati yuko kwenye hatua za kuja nyumbani sijui niseme bahati mbaya ama ni nzuri yule kaka Alifariki,, ilikuwa kama ghafla tu

Katika maisha yangu nishaumia na mengi ila hili jambo ni jambo linalo niumiza sana yaani mno… nimejitahidi kulikubali na nikajifanya nina nguvu ya kulikabiri, mbele za watu najifanya ni strong sitaki kulialia ila ndugu zanguni ni uongo ninalia sana na nina umia ndani kwa ndani kila nimkumbukapo huyo kijana

Tangu tatizo linipate sijawai kupata mtu wa kunifanyia counseling wala maombi.. sijawahi kuonana na mtu yoyote wa kidini ambae labda angeomba na mimi

Hata nikitaka kuomba mwenyewe siwezi nakosa kuomba nakosa maneno ya kuongea

Ubaya zaidi tangu huyo kijana afariki mimi kwangu mahusiano ni changamoto kila ninaempata ninafanya comparison sana kiasi kwamba najikuta naachwa achwaa

Kwa sasa nina mahusiano mapya yana miezi 5 angalau kuna ka mwanga lakini nahisi huyu Kijana atanichoka maana nampa pressure sana.. asiponitafuta nakuwa naogopa,, siogopi kuachwa naogopa nisije pewa taarifa za msiba

Hili jambo linanitesa sana hofu ya kuachwa imenitawala… hata kuolewa naogopa maana kila nikikumbuka kuhusu ex wangu marehemu inaniuma sana
Unajua Hakuna kitu kinaniuma kama kifo chake.. yaani mwanaume niliekuwa nampenda tunapenda yupo tayari kunioa.. baada ya mawasiliano ya masaa mawili napewa taarifa ya kifo chake
Mwanaume ambae tulipanga mipango mingi ya baadae…nilishaamini kuwa angeenda kuwa mme wangu,, baba wa watoto wangu,, niliacha kila kitu changu kwaajili ya kujiandaa kuwa mke wake

Unajua namna inavyouma 😭😭
Ni kama vile nilipokonywa tonge mkononi

Nahitaji kupata ushaurii wowote haswa wa kiimani
NB:
Naomba ushauri wa kwenda kwa manabii ama mitume ama watu wafananao na hao sihiitaji… siitaji kulishwa keki wala mafuta wala chumvi wala kitambaa.. sihitaji waganga wa kienyeji

Mimi ni mkristo kabisaa
Nahitaji kupata mtu wa kweli wa Mungu anaeongea na Mungu direct najua Tanzania nzima hatokosekana
Pole sana.titazo lako inaonyesha ulipenda kupitiliza ndio maana hiyo hali kukuisha ni ngumu sana .na dawa yake umpate mwanaume wa kukupeti (kukupenda kupitiliza) kiasi kwamba usahau yule marehemu.hapo wala auhitaji maombi ni kumwomba tuu mungu akupe wa kukupenda
 
Asa
Pole sana.titazo lako inaonyesha ulipenda kupitiliza ndio maana hiyo hali kukuisha ni ngumu sana .na dawa yake umpate mwanaume wa kukupeti (kukupenda kupitiliza) kiasi kwamba usahau yule marehemu.hapo wala auhitaji maombi ni kumwomba tuu mungu akupe wa kukupenda
Asante mkuu
 
Yaan wewe shukuru mungu huyo mtu amefariki, angekucheat ukiwa hai ungejinyonga

Mtu unaona kaburi lake bado unaumia eti mpenzi anakuuma

Acha hayo mambo, ukifika 30 utapona mwenyewe
 
Sadaka huweka mtu huru dhidi ya uraibu au machungu fulani!

Toa sadaka kwa hao waombaji na taasisi zao!ukiwa peke Yako chumbani mwambie kwamba "Kwa sadaka Ile ya sh ..... Kadhaa naomba unisaidie moja ,mbili,tati"SEMA ukimaanisha utapata amani pia mwenza utapata!!
 
Hakuna mtu anayeweza kuongea na Mungu direct kwa niaba yako. Huyo hayupo.

Mungu ashindwe kukusikiliza wewe amsikilize mtu mwingine? Hapo unaenda kupigwa.
Shikilia imani yako hiyo hiyo huko unapoabudu tafuta mtu mzima wa kukushauri. Sali kivyakovyako.

Tatizo lako lingine unawaza sana kuolewa nadhani unahisi muda umekutupa mkono. Haipo hivyo.
Tambua ya kwamba ex alifariki bahati mbaya na amemaliza kazi yake hapa duniani unapaswa kumsahau na kumove on.
Usiharakishe kuingia kwenye mahusiano mapya jipe muda, jikeep busy na mambo mengine mchumba atakuja kwa wakati wake.
Nakazia
 
Back
Top Bottom