Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Una wazazi?
Sungumza nao... Kama kuna wanacho kijua kuhusiana na jambo lako watakwambia... matatizo mengine yaaweza kuwa yapo kwenye familia...maagano ya wazazi au mababu halafu mnakuja kuyabeba bila kujua....

Familiar ya alie fariki unaifahamu vizuri? Au inaweza kuwa ni siku yake tu imefika akaondoka.....usibebe mizigo usiyo na uwezo nayo...utajiumiza na kufa kabla ya muda....
Hao wazazi wangu wanaoamini mambo ya mikosi sitaki kuzungumza nao maana mpk kufikia kuandika humu ni wao wanao nijaza hizo negative

Nilishaamini kwamba kifo ni Mungu alipanga Kama ni ushirikina mimi sitaki kufahamu

Ukoo wao siwafahamu kiundani
 
Chanzo nachoongelea hapa ni chanzo cha kiroho cha yeye kufariki.

Pengine alikuwa na uadui ndio ukamuondoa kupitia ajali, au pengine wewe ndio unauadui unaokuzuia usiolewe.
Kwangu hakuna uadui wowote labda kwao

Maana kwenye msiba mama yake alikuwa anawalaumu huko kijijini kwao kwamba wanemchukua mtoto wake
 
Hao wazazi wangu wanaoamini mambo ya mikosi sitaki kuzungumza nao maana mpk kufikia kuandika humu ni wao wanao nijaza hizo negative

Nilishaamini kwamba kifo ni Mungu alipanga Kama ni ushirikina mimi sitaki kufahamu

Ukoo wao siwafahamu kiundani
Hicho walicho kwambia ndo uingie nacho kwenye maombi...jiombee mwenyewe...omba mpaka upate wepesi... possibly kuna mikosi kweli au uoga tu vyote viondoe kupitia maombi.... Unadhani mtumishi akikuombea atakwambia nini?
 
Labda nikimueleza namna navyojisikia nikalia akanipa ushaurii na kuniombea labda nitapona
 
Polee sanaa, hii hali ilinikuta mie kipindi fulani.
Nilikua na mtu, yule wa kushibana nae, kwa kifupi alifanya nione dunia nyepesi kwa upande fulani, kunisaidia kwa hali na mali, sijui nielezeje. Hatukua na mahusiano ya kimapenzi, ila mie nilikua na hisia nae, ile kumfungukia ndo nilishindwa.

Alikufa kwa ajari ya piki piki, kile kifo chake kilinitia kiwewe, yaan nlikua napitia wakati mgumu hatari, shida wa kumueleza situation ile na akaelewa, sikumuona.

Baadae niliamua kuwa wazi juu yangu, ku ukubali ukweli na kuacha maisha yaendelee.
Nilipona kwa kiasi chake had now.
Nashauri kubali ukweli, na epuka kumuwazia sana huyo ex, japo sio rahisi, ila amini hivyo na maisha yaendelee.
Kwa hiyo ulishindwa kumfungukia kabisa?
 
Back
Top Bottom