Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Ushauri utakaokusadia:

1. Mwamini Mungu sana
2. Soma Biblia mistari ya faraja sana
3. Achana na mitandao.
4. Badili mfumo wako wote wa kufikiri

Hakuna mtu atakusaidia kwenye hili
Ok Asante
 
Pole sana binti usikate tamaa. Jaribu kumuomba Mungu ukiwa mwenyewe, usijiwazie mabaya waza vitu positive.

Ukishindwa nenda kwa Mchungaji Mwakasege kama upo Dar, huyu nasikia hana mambo ya mafuta na maji, anatumiwa na Mungu atakusaidia
Sawa Asante sana
 
Soma zaburi 51, alafu omba Toba na Rehema kwa ajili yako na ya mpenzi wako...

Kuna Roho ya mauti kwa ukoo wenu, hivyo omba Toba na Rehema pia kwa ajili ya familia upande wa baba na mama...

Utasahau yote

Utaolewa, Mungu ni mwema...
Amen mama mchungaji
 
Sawa Asante
 
Ni hivyo tu basi watu tunatofautiana lakini siku zote kama jambo halipo kwenye uwezo wako usiliwaze sana, Dili na unavyoweza kufanya. Tatizo ni mindset na wanawake huwa ni watu wa hisia sana.
 
Hilo ni tatizo dogo sana, linatokana na mindset uliyonayo na mazingira yanayokuzunguka. Ukiweza ingia Youtube tafuta mafundisho ya Pastor Tony Kapola, then utakuwa sawa!..
 
Sahihi kabisa
 
Kwanza nikupe pole kwa masaibu yaliyokupata,ambayo ni kudra ya Mungu na wajibu wako ni kumshukuru Mungu kwa kila kitu.
Sasa kwa hiyo shida uliyonayo,atakayeimaliza ni wewe mwenyewe kwa maombi kwa Mola wako bila kupitia kwa mtu yoyote yule,kama ulivyoambiwa hapa kuwa Mungu hana dalali.
Usimkufuru Mungu kwa kifo cha huyo mpenzi wako.Usilie sana na kuchanganyikiwa utadhani kuwa kazi ya ya Mungu ina makosa,mwambie Mungu asante sana kwa kunipa huyo mwanaume na asante sana kwa kumchukua,Mola wangu naomba mtu mwingine na atakupa.
Endelea na maisha yako,usiendekeze hofu wala woga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…