Nay wa Mitego amekanusha madai ya Mange Kimambi kwamba amelipwa Milioni 100 na muda wowote atatangaza kuhamia CCM
"Unaona mimi ni wa million 100 kweli.?! career yangu ina thamani kubwa sanaaaa, mapenzi ya Wana Nchi wangu huwezi fananisha na kiasi chochote cha pesa, na nina enjoy kua ivi nilivyo na Watu wangu. Siwezi kua Chama chochote coz mimi sio mwanasiasa bro"
Mange Kimambi adai Nay wa Mitego kahamia CCM baada ya kupewa milioni 100
Kupitia pags zake, Mange amedai Nay wa Mitego amejiunga rasmi na CCM na kupokea shilingi milioni 100 taslimu, fedha ambazo alipewa moja kwa moja na Abdul kutoka ofisi ya Rais Samia. Anadai mameneja wa Nay waliotarajia kupata asilimia 10 ya malipo hayo hawakupewa chochote baada ya Nay kuwazima.
Pia amesema Nay tayari ametengeneza wimbo wa kumsifu Rais Samia unaosubiri muda rasmi wa kutambulishwa. Mange amewataka wananchi kuwaunga mkono viongozi wanaokataa kununuliwa kama Lissu, akisisitiza kuwa yeye ndiye mwanaharakati pekee mwenye platform kubwa ambaye bado hajasalim amri.