Nayaandika haya huku moyo wangu unavuja damu. Uchungu mwingi sana

Nayaandika haya huku moyo wangu unavuja damu. Uchungu mwingi sana

Naweza kuyasikia maumivu yako, hakika unaumia sana, kauli yako umeitoa kwa hisia sana.

Naelewa na nakuelewa, karibu PM
Huu uzi wako umenifanya nmelia sana kwasababu mimi pia nina tatizo kama lako na limenitokea ukubwani manyanyaso shuleni yalinitokea hivyo hivyo.Pole sana tusikate tamaa naamini ipo siku mungu atasikia kilio chetu na tutakuwa na furaha kama wenzetu
 
Fado, Hahaha apewe nn tena. Hii ofa ya Kizazi sana aisee, big up!
 
Habari za leo!

Nimefurahi na kufarijika sana kwa hakika nina matumaini ya kuishi na nina sababu ya kuishi.

Nimeweza kupata marafiki wapya kwa uchache na naamini watazidi kuongezekaZaidi.

Vilevile siwezi ficha masikitiko yangu, nasikitika pia kwa kuuona mwamko na mguso wa mioyo ya walio wengi ukipotea mithili ya chozi la samaki baharini.

Niliamini kwamba nitaona mabadiliko ya mioyo ya watu, ubinadamu na upendo wa dhahiri katika kuniunga mkono, lakini haijawa hivyo na sina haki ya kulaumu yeyote yule.

Mwisho nimejifunza pia kuwa dunia hii imejaa machozi,kuna watu huishi katika dunia ya peke yao na najisikia huruma juu yao,natamani ningeliwasaidia hata kama si kwa chakula basi hata kulia ningelia nao.

Baraka nyingi ziwe juu yenu nyote.

Ahsante.

ROBIN.
 
Masikini laiti kama nigeona hii msg mapema labda ningeweza kumsaidia kidogo kupunguza maumivu ya kudhihakiwa, kudharauliwa, kutothaminiwa na kukosa upendo kutoka kwa jamii iliyomzunguka.. Lkn nasikitika kuona kuwa nimechelewa..

Pumzika kwa Amani mdogo wangu umeondoka mapema huku ukionja machungu kutoka kwa watu uliowaamini.

Kila atakayesoma ujumbe wa kaka yetu huyu basi ajifunze kutomdhalilisha binadamu mwenzio, kuheshimu utu wa binadamu mwenzio, usitumie ukilema wake kumyanyasa nao... Mpe heshima yake km binadamu mwenzio, msaidie km unaweza na km huwezi mwambie ukweli...
 
Mpauko,
Ee Mungu, kwanini watu wengine wanateseka hivi?

Kwanini mwingine anaita mabilioni hela ya mboga? Ulituumba sawa kweli?! au wengine wawasindikize binadamu!
 
Back
Top Bottom