Habari za leo!
Nimefurahi na kufarijika sana kwa hakika nina matumaini ya kuishi na nina sababu ya kuishi.
Nimeweza kupata marafiki wapya kwa uchache na naamini watazidi kuongezekaZaidi.
Vilevile siwezi ficha masikitiko yangu, nasikitika pia kwa kuuona mwamko na mguso wa mioyo ya walio wengi ukipotea mithili ya chozi la samaki baharini.
Niliamini kwamba nitaona mabadiliko ya mioyo ya watu, ubinadamu na upendo wa dhahiri katika kuniunga mkono, lakini haijawa hivyo na sina haki ya kulaumu yeyote yule.
Mwisho nimejifunza pia kuwa dunia hii imejaa machozi,kuna watu huishi katika dunia ya peke yao na najisikia huruma juu yao,natamani ningeliwasaidia hata kama si kwa chakula basi hata kulia ningelia nao.
Baraka nyingi ziwe juu yenu nyote.
Ahsante.
ROBIN.