Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.
Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.
Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.
Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.
Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.
Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.
Msaada tafadhali.
Mkuu bora ww mimi at 30's nina mvi balaa kichwani hadi kero yaani.
Aisee, yani hata mimi nimelala usika, kuamka asubuhi nakuta uso umetelemuka!
Yaakh...balaa!
kunywa maji mengi.
Fanya mazoezi.
kula matunda kwa wingi mboga majani.
vitungu saumu,tangawizi, malimao,pili pili.
pia hizo nywele paka dawa nyeusi uzichonge vizuri.
Aging imetofautiana sana kati ya mtu na mtu, usije ukafosi aging ako ifanane na ndugu zako wengine au age mates wako mana kila mtu ana unique aging genes.
Unatakiwa uufurahie uzee wako kama ulivyoufurahia utoto na ujana pia.
Vyote vina raha yake.
Mimi nipo 30s lakini naonekana wa 20s na huwa sifichi miaka yangu na nina furahia na mvi zangu kidevuni.
Ukijitahidi kuficha uzee ndivyo unazidi kuzeeka sababu ya stress.
Ila usipojali uzee wako basi unakuwa kijana zaidi maana hujali.
Mwisho wa siku uzee au ujana unategemea na fikra zako
Dawa nzuri ya kupunguza speed ya kuzeeka,Anza Kula na kunywa supu ya kongoro angalau 500mls Kwa siku Fanya zoezi Hilo mwezi mzima njoo na mrejesho ikikufaa endelea nayo.
Mvi sio uzee. Pia kuwa at 40 bado wewe sio mzee. Uzee huanza at 70’s. Pia uzee ni fikra za mtu.
Mwonekano wa kuzeeka hutegemea mambo mengi ila kubwa ni nasaba (genetics).
Mazingira na mazoea yana mchango mkubwa kwenye kuleta uzee. Angalia life style yako:
Mazoezi ya mwili ni muhimu, uwe unafanya kazi ya kushurutisha mwili kama kutembea umbali mrefu, kucheza mpira, kuogelea, nk itakusaidia.
Angalia unakula nini. Kula sana matunda na mboga za majani fresh. Acha junk foods kama chips na vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi.
Pumzika vya kutosha, lala walau masaa 7-8 kila usiku.
Punguza stress za maisha.
Acha mwili upigwe jua la kadiri, ngozi hutengeneza melanin ambayo huzuia kasi ya mvi.
Acha au punguza sana pombe na sigara.
Usile na kujaza tumbo kila wakati. Mwili huchoka na sumu huwa nyingi mwilini. Kula mara moja tu kutwa.
Punguza kula nyama nyingi.
Kuwa mwenye furaha wakati mwingi.
Jikubali uzee ni heshima!