Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msikaririshane, kwa afya ya ngozi kikanuni ni;
1. Maji ya moto jioni/usiku ili uoge ulewe ulale
2. Maji baridi asubuhi ili uoge uchangamke ukafanye kazi.
Kila kimoja kina sehemu yake, na vyote moto na baridi vinahiyajika kwa wakati wake. Imfikie na Depal
Ona mwamba, yote nnayoandika ni nadharia. Ntafurahi nikipata majibu toka kwako.Kama umenielewa vzr sijaforce chochote mtaalamu wewe, nimeshangaa tu inakuaje kimuonekano nawa'level' na hata kuwapita kwa mbali makaka zangu, mababa wadogo walio miaka 10 mbele yangu na age mates wengi tu.
Kumbe siku hz hakuna utu uzima ee?!!! Kuna utoto, ujana halafu uzee.
Nimekubali mtaalamu 👏Mimi nakujibu kitaalam Hiyo kukaririshana Utajua pakuiweka.
Nadhani ningesema kwanza maji yanaweza kuwa ya moto(joto kali), vuguvugu(joto la wastani), no baridi( joto dogo)..na ninadhani katika thread/kwa ujumla watu husema maji ya "uvugu vugu" wakimaanisha maji ya "moto", kitu ambacho si sahihi sana.Uchaguzi wa kuoga kwa maji ya baridi au yenye joto kiasi hutegemeana na "utashi" lakini pia hutegemea;
Umri: Wazee na watoto wadogo maji ya uvuguvugu ni mazuri zaidi, na baridi kwa vijana.
Magonjwa: Baadhi kama Ini, wenye matatizo ya burning sensation maji ya baridi hufaa na wale wenye mafua, allergy, maumivu ya vifundo, kikohozi kwao ya uvuguvugu ni bora zaidi.
Msimu: Wakati wa baridi ni vizuri kutumia maji ya uvuguvugu, na wakati wa joto kutumia maji yenye ubaridi.
Tabia: Yaani wale wanaofanya mazoezi na wasiofanya mazoezi.
Lakini hata hivyo, kiafya hakuna madhara kwa watumiaji wa maji ya uvuguvugu...hata hivyo kwa maji ya MOTO unaweza kupata madhara kadhaa.
1. Kuharibika kwa ngozi: Mwili huweza kuhimili joto na kwa wenyewe(mwili) kujitbadilisha ili kujihifadhi(regulate) katika mazingira tofauti, hata hivyo joto likizidi na mwili ukashindwa kustahimili, ngozi huharibika mf. kuungua, kubabuka n.k
2. Magonjwa: Katika ngozi, vinyweleo husaidia sana katika "kubadilisha" joto kulingana na mazingira(regulate), na hivyo basi endapo maji ya moto(si vuguvugu) yataendelea kutumika mara kwa mara huweka kuharibu sehemu ya vinyweleo na ngozi kuonekana ipo nyekundu, muwasho,na huweza kupasuka( Hot tub/bath Folliculitis)...hii ni kutokana na joto kali(Heat rash)..mf. mzuri ni watu watokapo sehemu ya baridi wakijaribu kuishi sehemu ya joto..au hata sehemu zenye joto mf. Dar na joto likaongezeka watu hapata "Heat rash" pia...Tatizo hili huisha lenyewe ndani ya siku saba hadi kumi hivi.
3. Madhara kwa mtoto: Kwa wakina mama wajawazito, kutumia maji ya MOTO si vyema sana, kwani wakati wa ujauzito msukumo wa damu wa mama, huweza kubadilika kwa urahisi sana na kwa kutumia maji ya moto husababisha jotomwili kupanda,(overheated), huleta mapigo ya moyo kwenda kasi, kufanya msukumo wa damu kuwa mdogo na damu kidogo kutolewa hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto aliye tumboni.(mtoto ana kuwa in a stressful condition.)
Hivyo basi, kwa kutegemeana na sababu nilizokwisha sema hapo juu, uamuzi unaweza kufanya kwa kutumia maji ya ubaridi au uvuguvugu..na si maji ya MOTO.
Nimesahau kuaknowledge kunasehemu nimetoa aiseee..Nimekubali mtaalamu 👏
Dunia ibinukeMsikaririshane, kwa afya ya ngozi kikanuni ni;
1. Maji ya moto jioni/usiku ili uoge ulewe ulale
2. Maji baridi asubuhi ili uoge uchangamke ukafanye kazi.
Kila kimoja kina sehemu yake, na vyote moto na baridi vinahiyajika kwa wakati wake. Imfikie na Depal
Pitia pitia tena hapo we mwl wa math , Uone shule niliyotoa ukanitunuku sasaApuuzwe..🤣
😂😂 sijasoma hii comment..Pitia pitia tena hapo we mwl wa math , Uone shule niliyotoa ukanitunuku sasa
Shwaaaaaaaa.😂😂 sijasoma hii comment..
Kutelemuka ndio kufanyaje? 😆😆😆Aisee, yani hata mimi nimelala usika, kuamka asubuhi nakuta uso umetelemuka!
Yaakh...balaa!
Mashavu aliyaokotea shingoni labdaKutelemuka ndio kufanyaje? 😆😆😆
Anhaaaa hahah! Lakini wanasemaga wenyewe wanaume hawazeeki haraka! 🤷🏻♀️Mashavu aliyaokotea shingoni labda
Mkuu bila picha mkuu🤣🤣😂😂Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.
Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.
Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.
Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.
Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.
Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.
Msaada tafadhali.
Mimi na huyu jamaa hatuchekani.Kutelemuka ndio kufanyaje? 😆😆😆
Acha uongo mkuu! 😂Mimi na huyu jamaa hatuchekani.
Mimecheka nyie. Eti azeeke nani?Tulia hivyo hivyo usijitingishe unataka azeeke nani mkuu tena miaka 40 mzee kweli wewe