Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.
Yawezekana nakujua. Umeishi Kimanga? Ila muhimu sasa kuanza mazoezi haswa ili kuukakamaza mwili. Pia pendelea kunyoa kipara na ndevu at least hadi ufike 55+
 
Tatizo lako inaonekana umeanza punyeto ukiwa bado mtoto sana na bado haujaacha....Fanya mazoezi acha pombe kula mbogamboga matunda achana na wanawake au kupiga punyeto ovyo.
mzee green eeh!!,alaf umesahau ki2 kimoja,,,mwambie anywe pombe ya mnazi,,,,,,,alaf aache tabia ya kwenda kuloga wenzake,na apunguze wivu kwa wafanyakazi wenzake!!
 
Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.
kunywa maji mengi.
 
Utajongea tu kwenye huu umri na ww.
wala usitukane karibu sana. Au na ww kwako umri umeganda kama wa wema sepetu manake yule toka 2018 mpaka leo bado ana miaka 29
Nimetukana wapi???
Ni hivyo nani kakuambia nagandisha??
 
Dunia ibinuke
Ndo nioge maji ya baridi asubuhi
Kama huwezi yabaridi kabisa basi changanya na yamoto kdg kutoa ubaridi tu lakini yasiwe yamoto. na ikiwezekana usoni na kwa bibi Depal tumia maji ya baridi, yale ya bombani. kwa uso kama inawezeka tumia ya baridi hasa yalowekwa kwenye friji. uso wako kila siku utaonekana wa kijana
 
Hizo tips zimwage hapa hadharani na sisi tujifunze
Mkuu, unakumbuka story ya Elisha na Naaman ktk Agano la Kale?

Elisha alimwaambia Naaman kuwa atapona ukoma akienda kupiga mbizi mara saba ktk mto Yordan. Mto huo hadhi yake ya usafi haina tofauti na mto Msimbazi au mto Ng'ombe unaokatiza Mwananyamala.

Nakupa simple tips hapa, fuata link hii hapa Thread 'Miujiza kuhusu Therapy ya bamia' Miujiza kuhusu Therapy ya bamia

Ahsante
 
Back
Top Bottom