Nazunguka hapa JNIA, sijaona mkusanyiko wa aina yoyote

Nazunguka hapa JNIA, sijaona mkusanyiko wa aina yoyote

Status
Not open for further replies.
Niko nazunguka zunguka hapa JNIA, Kwenye shughuli zangu lakini pia niko naangalia mikusanyiko ya watu kama wapo sioni dalili ya mkusanyiko.

Maana yake mambo ya wahamasishaji wa mitandaoni kutokutii mamlaka za nchi zimepuuzwa wananchi wako kwenye msiba mzito na maombolezo ya Kitaifa.

Wananchi wameielewa Serikali na wanaitii serikali yao ningeiomba serikali isimsumbue Tundu Lissu ili CHADEMA wamuweke kuwa mgombea wao ili tuone kama atapata hata diwani mmoja.

Na nina uhakika akikosa diwani hata mmoja ili baada ya uchaguzi akiwa na aibu ya kushindwa kesi zake zianzie hapo hapo.

Ahsanteni sana watanzania kwa kuendeleza jadi yetu.
Pole mkuu! Umeandika Uzi kwa uchungu sana. Achana na shughuli zisizokuhusu, hata hiyo kuna aliekuomba utoe taarifa za mapokezi ya Mh. TAL.Kupitia
TAL imani za wengi zimeongezeka kwa utukufu wa Mungu mwenye kutenda miujiza.
 
Sure...

Kweupeeee....

Anaonekana Sugu na Heche,Cathy Ruge na Yule wakili wao...
Huku KARAKATA Kimyaaaa......
Makomandoo wa Mitandaoni 😂😂😂😂😂😂
 
MACHALE YA JESHI LA POLISI, GODBLESS LEMA, CHADEMA NA MIPANGO HARAMU ILIYOFELI:

#Nanukuu : "Sina amani kwa tabia nzuri waliyoonyesha Jeshi la Polisi jana wkt wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu.Nina paswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari,kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi - Godbless Lema.

MYTAKE :

Ukisikiliza Maelezo ya Hovyo toka kwa Lema na Kwa akili za Ufipa Street utaona kabisa walitamani Wadundwe, Watawanywe kuliko kuachwa...Hawa Walijiandaa na Walishajua kuwa Askari Watafika na kuwatawanya kama ambavyo Barua ya Polisi ilivyoainisha!..So kutofanyika kwa jambo hilo kumeharibu kabisa Mipango wa Maharamia hao,...Hii haiihitaji Betting, kifupi Mpango ulikuwa hivi:

Polisi Wangeingia Kati na kutawanya Mkusanyiko wa Chadema pale Airport basi kama kawaida Chademaa ingetumia Special Unit ya vijana wake maalumu ambao wangejichanganya katikati ya Mkusanyiko wa Nyumbu na kufyatua risasi zinazoweza kudhuru raia na kuzua GUMZO la violence na Msala kuangukia kwa jeshi la Polisi..."Hii inaitwa "Nyumbu kudhuru Nyumbu"..Special unit hii ya vijana hawa inasemekana ndiyo miaka ya Nyuma ilitumika kupiga mpaka Mabomu ya Moto katikati ya Mikusanyiko ya Chadema pale Arusha ikiwajibu polisi waliorusha "Mabomu ya Machozi"...Raia Wakafa! Jumba Bovu kwa Polisi.

Siasa za Kilofa Hasa!... Dola nyingi Afrika kwa kutokushtuka Mapema zimenasa katika mtego huu, polisi wengi wamenasa ktk Mtego huu na kujikuta too late ktk kujinasua...na inasemekana vikundi hivi Maalumu hupokea Mafunzo na Posho kwa ajili tu ya kuleta taharuki ndani ya Mikusanyiko mbali mabali haramu, Vikundi hivyo vipo tauari hata kama ni kwa kumwaga damu ya waandamanaji na finally Nchi husika kuingia katika Machafuko kama Tunisia.

Nikumbushe tu kwamba Tarehe 19 september 2018 Taifa likiwa ktk uchaguzi Mdogo Jeshi Polisi lilimkamata Wakala wa Chadema ndani ya Chumba cha Kura akiwa na Barua Feki, Furushi la Nyuki na Bastola yenye Risasi 15 .

Probably Malengo ya Wakala yule yalikuwa kuanzisha Vurugu eneo la uchaguzi na kwenye Mkusanyiko wa watu kisha amwage Nyuki, Watu wakiwa wanakimbia hovyo hovyo na Askari kujitokeza kutuliza Ghasia ndipo Wakala huyo angetumia Bastola hiyo kutandika Risasi Raia mmoja halafu Kesi inakuwa ya Polisi, Lawama kwa Serikali, reporters ni DW, BBC na VOA....Yale Yale ya Kinondoni kwa Akwilina na Mabomu ya Arusha....Hawa ni watu wa Matukio na nina Hakika Kauli ya Lema inapaswa kufikiriwa zaidi na kufanyiwa kazi zaidi, ni kauli iliyotangulizwa tu huku Matukio yakiandaliwa!.
 
Kwanza ningemshauri awaambie viongozi wake wa chama waje na gari moja tu la kumpokea.

Angepokelewa kimya kimya akaenda ofisi za Chama na kuwasalimia viongozi wa Chama.

Angetoa maneno ya shukrani kwa mwenyezi MUNGU na angewapa pole watanzania kwa kuondokewa na Rais mstaafu yaani angeonekana kuguswa na tukio la msiba.

Angekaa kimya bila kutoa hoja zozote gawanyishi mpaka msiba uishe.

Angesubiri uchaguzi ndani ya Chama.

Angetoa hotuba kama Mgombea Urais.
 
Kila mada mtaandika mwaka huu.

Tatizo lenu mnatumia hisia badala ya uhalisia.

Kwani kumpokea ndugu yako ni kosa?

Ni mara ngapi CCM wanawapokea watu wao na hatuoni policcm wakiwasumbua?

Hawakupenda patokee vurugu lakini sikawaida yao policcm wasiwasumbue na kuwapiga chadema.
 
Kwa jinsi alivyopita na kutoka katika bonde la uvuli wa mauti ametangaza utukufu wa Mungu. Chochote kumuhusu yeye kwa sasa ni kushangilia hilo. Mashetani yameshindwa.
 
Hawa ni wenye kukaanga mbuyu kama kina musiba tu.

Hawana umuhimu wowote, ni wa kupuuza na zaidi kujipanga kutokuwapa vijivinafasi vya kupenyezea propaganda zao.

Mbona mtanzania wa leo si wa jana?

Washindwe na walegee!
 
Umejifunza nini kwenye hadithi hii?
-Makonda kutia nia ni mkakati wa ndani bila mwenyewe kujua. Baba alionya mara kadhaa asithubutu,lakini akawa na roho ya farao. Atakuwa kama Mwananzila,hata ukatibu kata hafai;haridhiki.
-RC mpya Dar amekuja na siasa za kistaarabu
-CDM walijiandaa kwa shari,(waliaandaa press release)lakini wakakutana na akili kubwa.
-Walitaka kick kwenye msiba wa kitaifa,ikabuma. Walikosea protokali. Viongozi waliaandaliwa usafiri wa pamoja,wao wakaja na usafiri binafsi.
 
Kwa hiyo Chadema wana 'special unit' ya kigaidi ambayo ww unaijua na polisi wanajuwa lakini lakini imeachwa tu ieendelee kuwepo? Kwa maelezo yako uniti hiyo ndio ilimuuwa Akwilina, na serekali ipo na haikuchukua hatua yoyote? Mtu mwenye akili mgando ndiye atakuamini.
 
Umejifunza nini kwenye hadithi hii?
-Makonda kutia nia ni mkakati wa ndani bila mwenyewe kujua. Baba alionya mara kadhaa asithubutu,lakini akawa na roho ya farao
-RC mpya Dar amekuja na siasa za kistaarabu
-CDM walijiandaa kwa shari,(waliaandaa press release)lakini wakakutana na akili kubwa.
-Walitaka kick kwenye msiba wa kitaifa,ikabuma. Walikosea protokali. Viongozi waliaandaliwa usafiri wa pamoja,wao wakaja na usafiri binafsi.

Mkuu binafsi nilikuwapo msibani jana na hata JKNIA juzi kama mtanzania Mzalendo. Utakuwa na nini cha kuwaambia watanzania wewe?

Nimeshindwa kwenda Lupaso lakini ningewakilisha kule pia. Kwa dhati kabisa.

Rais alipolia, hakulia peke yake. Tumelia wengi. Achilia mbali wenye machozi yenye kuingia ndani.

Waliokuja kumuaga mzee Mkapa ambaye ni Rais wetu, mtanzania mwenzetu na binadamu aliyetutangulia wanastahili shukurani na faraja toka kwa walio na hekima lakini.

Kurejea kwa salama kwa Lissu si mchezo wa paka na panya. Ni furaha iliyoje aliyekufa akifufuka?

Tuwatambue kwa majina yao wote wenye nia ya kutugawa, kwa hakika tuwanyime nafasi hiyo.

Hata mzee hajazikwa mmeanza? Watu wa namna gani nyie?

Au yale yale ya: "tunatoana roho, Yarabi. Kwa mali alizoacha baba."

Tuwakilishane Lupaso.

Apumzike kwa amani Muhidini Mwalimu.

Apumzike kwa amani mzee wetu Mkapa.
 
Kila mada mtaandika mwaka huu.

Tatizo lenu mnatumia hisia badala ya uhalisia.


Kwani kumpokea ndugu yako ni kosa?

Ni mara ngapi ccm wanawapokea watu wao na hatuoni policcm wakiwasumbua?

Hawakupenda patokee vurugu lakini sikawaida yao policcm wasiwasumbue na kuwapiga chadema.
Na Walijipanga kupigwa wakati wamejipiga wenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom