Nazunguka hapa JNIA, sijaona mkusanyiko wa aina yoyote

Status
Not open for further replies.
Ina maana chadema walikuwa na mabunduki ya kivita, mbona hayakuonekana. Huu ni upotoshaji. Hivi kina Akeilina walipigwa na silaha zilizofichwa kiunoni?

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mnahangaika sana hakuna mada nyingine? Andikeni hata kuhusu Fly overs
 
 
Mimi nafikiri askari wetu kuacha maandamano yale yaendelee na huku wakiwasindikiza, ilikuwa namna ya kumwenzi Hayati BWM kwa yale aliyokiri katika kitabu chake kuwa mauaji yaliyotokea Pemba wakati wa uchaguzi, hayakumfurahisha. Isingekuwa vema wakati tukiomboleza msiba wa rais wetu mpendwa kukatokea bahati mbaya kama ya Pemba au Kinondoni (Akwilina). Kwa hiyo ni faraja sana kwa Hayati BWM kuwa ameenziwa kwa toba aliyotoa kwenye kitabu chake na ni vizuri uhuru huu uendelezwe kwani tuliwaona askari wetu wakiusindikiza msafara kwa amani na hakuna uvunjifu wa sheria wowote uliotokea.

Na kwa kuenzi huko, hatutarajii kuona uanzishwaji wa kesi yoyote kuhusu mapokezi hayo ya M/Mwenyekiti wa CHADEMA. Mungu ibariki Tanzania yetu iendelee kuwa na amani.
 
Ni zezeta tu wa kukuelewa we jamaa. Hujaona chadrma wanavyppost kulisifu jeshi la polisi kwa kucmamia haki?

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kumbe dawa yao imepatikana nayo ni hii: KUWAPUUZA M4C!
 
-RC mpya Dar amekuja na siasa za kistaarabu
Wewe unaamini agizo la kuwaacha CHADEMA wampokee Lissu bila kusumbuliwa lilitoka kwa RC?
Kweli hivi unaweza kuamini ana nguvu hizo bila amri kutoka juu?
TAFAKARI ....
 
Wewe unaamini agizo la kuwaacha CHADEMA wampokee Lissu bila kusumbuliwa lilitoka kwa RC?
Kweli hivi unaweza kuamini ana nguvu hizo bila amri kutoka juu?
TAFAKARI ....

..askari waliokuwa on the ground waliona umati ule ni mkubwa mno, na kuutawanya kungeleta madhara makubwa.
 
..askari waliokuwa on the ground waliona umati ule ni mkubwa mno, na kuutawanya kungeleta madhara makubwa.
Kwa miaka iliyopita ule umati inawezekana kabisa kuutawanya na wenye majukumu na dhamana wasijali madhara yatakayotokea.
Sasa hivi tochi zimekuwa nyingi sana, wameogopa kumulikwa na kuchafuka ulimwenguni kote, watu wangepata sababu ya kuiwekea nchi yetu vikwazo au kufanya yale ya Libya.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…