DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mlikuwa mkishusha nyuzi Sana humu Tena mkatutukana walimu wenu eti tuna roho mbaya ...Sasa sikieni nyie makarani ...sensa itaisha na mitaji hamtapata hela mtapewa 200 ,miambili mpk itaisha ..hiyo ndio serikali...!!!
 
Sasa ya safari hii sijui kama itabeba uhalisia maana dereva ameota mapembe
 
Umeandika mawazo yako kwa hisia zako tu, kama na wewe ni mmoja wa waliofurushwa kutokana na kufeli mafunzo usilielie….. malipo siku zote ni baada ya semina.
 
Kwa zile kauli za Anne Makinda sijui ngoja tuone. Maana waru wanapiga hesabu za kukunja 1.3M lakini sidhani.
Unategemea nini kutoka kwa Anne Makinda? Watu wale waleee, chama kile kileee..., CCM ni ile ileee! Eti kauli, jamani kuweni serious, oneni aibu japo kidogo.

KIjana wa watu anahudhuria semina kwa zaidi ya wiki, hapewi hata senti tano. Baada ya wiki anafukuzwa kama mbwa, halipwi hata senti tano.

Vifaa walivyotakiwa kupewa kuwawezesha katika semina vimeota mbawa. Je hivyo vifaa viko wapi. Sasa wanatakiwa watumie simu zao, jameni oneni aibu.

Vijana wanateseka, nauli zimepanda...hakuna pesa, hakuna vifaa, hicho chakula...wewe acha tu. Wamewakosea nini hawa vijana msikini? Kuweni japo na huruma!
 
Zoezi la postcode liliharibika hivi hivi. Hadi leo mahali napoishi namba za vibao zimeandikwa kwa mkaa ukutani. Waliofanyakazi ya posti kodi wanadai zaidi ya laki moja posho yao ilifia huko huko halmashauri X
Kuna watu walifanyakazi ya chanjo ya polio hawajalipwa hadi leo, THIS IS TZ

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Mlikuwa mkishusha nyuzi Sana humu Tena mkatutukana walimu wenu eti tuna roho mbaya ...Sasa sikieni nyie makarani ...sensa itaisha na mitaji hamtapata hela mtapewa 200 ,miambili mpk itaisha ..hiyo ndio serikali...!!!
Sasa ndugu mwalimu mwenzangu unafurahia hawa vijana kutapeliwa au kulipwa kidogokidogo ili wasipate mitaji?kuwa na huruma na hawa wazalendo
 
Sensa ya mwaka huu ni majanga tu. Wanasema mtu atahesabiwa pale alipolala usiku wa kuamkia 23.8.2022; lakini hawaelezi ni taarifa zipi mtu aziache ili wakija hata siku ya pili wazikute. Labda kama huko mijini mnajua. Kwa hiyo mimi nikilala nyumbani kwangu kisha nikaondoka, sijui ni kitu gani watamuuliza wife wangu. Na kama kuna mgeni amelala, sana sana naweza kuwa najua jina lake tu
 
Umeandika mawazo yako kwa hisia zako tu, kama na wewe ni mmoja wa waliofurushwa kutokana na kufeli mafunzo usilielie….. malipo siku zote ni baada ya semina.

Mitihani watu wamepata 100% sasa sijui hoja yako nn?!
 
Mi kwa kauli hii ya huyu mama sidhani kama watu hawajapigwa hapa.
Aachane na mambo ya uzalendo, hii ni moja ya njia ambayo serikali inaweza kuingiza pesa kwenye mzunguko na yenyewe ikawa imefaidika na hilo zoezi kufanyika kwa ufanisi, labda waseme hawakujiandaa kwa hiyo miaka 10.
 
Back
Top Bottom