Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wanasema barabara ya kuzimu imesakafiwa kwa nia njema. Watu wanaopinga mauaji yanayofanywa na polisi kwa washukiwa wa uhalifu wana nia njema sana. Na ni kweli kuna polisi waovu na wanatakiwa kudhibitiwa na kushughulikiwa. Lakini hili ni suala la kuangalia kwa makini sana.
Ukishaanza kuwabana polisi kwa kisingizio cha ubinadamu huwa haina kurudi nyuma, utawabana hiki, kitalalamikiwa kile utawabana. Utawabana utawabana. Mwisho utajikuta umewapotezea kabisa uwezo wa kutenda kazi kwa ufanisi. Hapo ndipo nchi zinaingia kwenye uhalifu usiodhibitika. Polisi wataacha kujali kushughulikia uhalifu kwa kuhofia taratibu zinazowabana.
Kumbuka wahalifu wengi hawana habari na haki za binadamu. Wao kuwabana polisi kwa kigezo cha haki za binadamu ni nafasi ya kutenda uhalifu wao vizuri.
Polisi na haki za binadamu ni suala tete, linahitaji umakini mkubwa sana.