Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Nchi imekuwa ngumu kuliko hata awamu ya 5 , tofauti kidogo ni yale mambo ya kutekana tu , lakini kwenye hela na uchumi nchi kwisha kabisa !
 
Aziuze milioni 6 inatosha kulima ekari moja na nusu ya nyanya ruaha mbuyuni ,anaweza pata hata milioni 30 ambayo ni pesa ya maana
Mkuu hizo hesabu za eka moja ya matikiti inakupa million 30 nilishaachana nazo muda sana. Niliamua kulima zao lenye risk ndogo ya kupoteza kabisa baada ya kuandaa Shamba langu kwa muda mrefu....kwenye karatasi inawezekana njoo Shamba sasa ujionee. It takes everything to get at least something..
 
Mi pia ni mkulima mkuu nina uzoefu miaka minne naelewa ,horticulture ni gharama ila unalima eneo dogo unaloweza kumaintain,achana na mahindi,
 

Mahindi sio chakula cha binadamu pekee ila kwa Tanzania zaidi ya 90% ya mahindi tunategemea yaliwe na watu!!
Mahindi ni chakula kizuri cha mifugo kama kuku, ngiuruwe, ng'ombe hivyo kama tunataka kulima kilimo cha mahindi cha biashara tuanzishe miradi mikubwa ya ufugaji hatutapata shida ya soko la mahindi.

Zaidi ya 70% ya watanzania ni wakulima (peasant) kila familia inlima mahindi yake, unalima mengi kumuuzia nani? Hata ukisema upeleke Kenya, Uganda, Rwanda n.k nao wana peasant kibao. Kilimo bado ni kazi ngumu nchini kama wananchi wataendelea kukaa vijijini bila tija kiuchumi (urbanisation is the way)
 
Hali ni mbaya chief,hata mie naiona,
Tabaka tawala,halina majibu kabisa,hivi kweli kilo ya mahindi iuzwe shilingi 500!huyu mkulima atajenga vipi nyumba,atasomeshaje mtoto chuo kikuu,ataweka vipi akiba ya uzeeni?
Miaka 60 ya uhuru nchi haiwezi kuwahakikishia wakulima bei nzuri ya mazao yao!!
Hii ni shida,sasa hv kila kijana anaenda kwenye kilimo,wakati ilibidi wakulima wawe wachache,vijana wengine wawe kwenye viwanda,hii ni balaa,
Serikali inahangaika kuajiri polisi wengi!!Ili waje wakuze uchumi?!!
Haki ya Mungu,natamani kukimbia hii nchi,kwa vijana ambao hamjawa na familia na huko na Elimu nzuri,tafuta passport,ukiona fulsa nje,sepa fasta
 
Uko sahihi,huwezi kutoboa kimaisha kwa kulima mahindi
 
Shida yote hii ni kwa sababu ya mifumo mibovu ya nchi hii chini ya utawala kandamizi wa ccm.
 
Shida serikali imejiingiza kwenye biashara hawawezi ruhusu..huoni wamefungua maghala south sudani na wanafugua kongo na komoro.

Mahindi yakiuzwa nje watapata wapi mahindi ya bure bure ili wakatengeneze faida huko nje ya nchi.
#MaendeleoHayanaChama
 
Uzi unafikirisha sana, yaan heka 20 mtu anapata gunia 200 basi ujue hapo gharama alizotumia ni kubwa mno,
Hilo la nursing pia upo sahihi, tuzidi kumuomba Mola muumba mbingu na ardhi

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Kilimo cha mvua ni upumbavu sana ndiyo maana wmnawaeshimu wakulima wa tz kuliko maprofesa maana wanafanya kazi ngumu sana hadi kuifanya tz kuwa na chakula cha kutosha hadi kuuzia nchi nyingine ,hapo kwa heka 20 kwa kilimo cha kumwagilia alitakiwa kupata magunia 1000 hadi 1200
 
Hatarii
 
K wenye karatasi ni sawa!
 
Shida serikali imejiingiza kwenye biashara hawawezi ruhusu..huoni wamefungua maghala south sudani na wanafugua kongo na komoro.

Mahindi yakiuzwa nje watapata wapi mahindi ya bure bure ili wakatengeneze faida huko nje ya nchi.
#MaendeleoHayanaChama

Hii serikali na sera zake mbovu itazidi kututia umaskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…