Mkuu Pagan Amum, ukweli lazima tuukubali na kuuheshimu kwama viongozi wa vyama vya upinzani, hasa wawakilishi wetu, hawakutenda kama tulivyowatarajia, katika kipindi cha utawala wa Serikali ya CCM.
√ Walipinga juhudi za maendeleo wakidai ni maendeleo ya vitu;
√ Mbaya zaidi walitumia lugha ya matusi, tuhuma za uzushi na kuhamasisha vurugu wakati wa kampeni; na
√ Isitoshe vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, chama kikuu, na ACT-Wazalendo, viliwekeza nguvu zao zote kwenye wagombea Urais, ambao walishindwa kuwashawishi wapiga kura kwa hoja za kisera.
Kama ulivyosema afya ya kisiasa siyo nzuri sana uwakilishi kuwa wa chama kimoja cha siasa. Lakini kumbuka, CCM ina jinsi nzuri ya uendeshaji kudhibiti na kusimamia utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi kuliko vyama vingine vya siasa, ambavyo viongozi wake wamekuwa wakishutumiana kwa matumizi ya ruzuku na mali za chama