Nchi kukaa muda mrefu bila Baraza la Mawaziri siyo Sifa, tafadhali teua Majembe ya Kazi Ufanisi uimarike Serikalini

Nchi kukaa muda mrefu bila Baraza la Mawaziri siyo Sifa, tafadhali teua Majembe ya Kazi Ufanisi uimarike Serikalini

Waziri awezi fanya kazi yake bila ya katibu mkuu. Hila katibu mkuu amuitaji waziri.

Serikali pia aiwezi fanya mambo yake bila ya makatibu wakuu, hao mawaziri maswali wanayojibu bungeni wanategemea wafanyakazi wa wizara ambao wapo chini ya katibu mkuu kuwaandalia majibu.

Usimamizi wa shughuli za wizara na utekelezaji wa sera zipo chini ya makatibu wakuu.

Policy za serikali zinashauriwa na makatibu wakuu, wanapozikubali wasimamizi wake ni makatibu wakuu.

Kesho raisi na makamu wakiumwa, kiongozi wa muda ni balozi kijazi sio PM.

Kwa kifupi ni kwamba mfumo wa serikali za madola makatibu wakuu ndio watu wanaoongoza nchi isipokuwa hawana ridhaa ya wananchi.

Si ajabu wengi awafahamu technically balozi kijazi ndio head of TISS pia wafanyakazi wote serikalini huyo ndio boss wao rasmi.
 
Ile kauli ya Zitto
'tumewapa nchi washamba na malimbukeni'
Ilikuwa kauli yenye maana sana
Ni kauli mbaya kwa viongozi wenye mamlaka.

Muulize yeye asiye mshamba amejifunza nini kwa washamba? Itoshe kusema ndio watoto wa mjini na wamemuingiza mjini.
 
Jamaa lenu lilivyo fisadi papa utakuta linakula hiyo mishahara ya mawaziri ambapo walipaswa wawe wameshachaguliwa kwa sasa.
Ndugu unafikiri taratibu sana, kwa Rais hiyo pesa ni ndogo sana na ana uwezo wa kutengeneza mazingira ya kupata pesa nyingi sana kama usinavyoweza kufikiri, lakini ni Rais mzalendo hana shida mshahara wake unamtosha
 
Sidhani kama ni Afya sana/ ni Sifa mno kwa Baraza la Mawaziri (Cabinet) kutoteuliwa hadi leo. Uliwataka Mwenyewe uletewe kwanini huwaamini?
Hakuna shida hao Mawaziri wa Magufuli ni wake mwenyewe akae nao wananchi hawakosi kitu maisha yanaendelea bila hiyo mizigo ya CCM na inadhihirisha kuwa tunaweza kuishi bila Serikali ya Awamu ya Tano mpaka Uchaguzi ujao baada ya Uchafuzi wa mwaka huu.
 
Jamaa ni kama anamuongoza ma Janeth na watoto wake, taifa lote linaongozwa kama anavyoongozwa ma Janeth hakyanani!
 
Mawaziri wanatakiwa waje na style mpya ya kuongoza...wabuni mikakati na mipango kwa kufuata dira za maendeleo zilizopo..Ilani ya chama na uelekeo wa Dunia.

Waziri wa Kilimo kwa mfano aangalie mazao gani ya kulima mkoa upi...changamoto na namna ya kuzitatua na kuimarisha mfumo wa kilimo hicho...Waziri wa Fedha aondoe kero za kodi..kuimarisha shilingi na uchumi jumuishi...Dhidi ya uchumi holela wa kila mtu kuuza kokote chochote...

Bahati mbaya sana wanaweza kuja na style ya matamko na kutumbua bila kuona athari zake matokeo yake anaoenea watu kwa chuki tu..na yeye akiondolewa basi anabaki kama Wengine.
 
Back
Top Bottom