Ipo hivyo yani wala hakuna haja yakuanza kujadili.
============================
=>Demokrasia inatakiwa kutumiwa na nchi zilizoendelea(boom stage) kama Korea kusini vile, madarakani wanakuwa kama wanacheza game vile, wanaangalia huyu kacheza kapata point ngapi, ngoja tuone mwingine atafikisha point ngapi?.
Sasa mfumo huu sisi hautufai ili kujikwamua kunamahali yatahitajika maumuzi magumu yenye manufaa baadae ila itashindikana kwasababu utakua nje ya mipaka ya demokrasia. Kwa kuukubali huu mfumo inamaana tumekubali kua wasindikizaji.
=>Demokrasia imeigawa nchi (integrity) ya wananchi ule uzalendo wa wananchi dhidi ya nchi yao umekimbilia kwenye vyama(uCCM & uCHADEMA) kipaumbele sio nchi tena bali ni vyama.
=>Hii demokrasia sio kwamba tulipigwa(tulitapeliwa) hapana bali tulikutana na vibaka, wakatupiga roba ya mbao wakatushikia visu na bisibisi kisha wakatuambia tusaule basi tukasaula.
☕️Kama tumefeli tayari basi mbadala uliobaki ni kutengeneza katiba yetu saaaafi kabisa itakayotutetea.