Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Ndugu yangu Katiba na sheria tulizojiwekea wenyewe ni muhimu zikafuatwa na katiba ndio mkataba wetu kati ya watawala na watawaliwa ndio the mother law of all laws, sasa ni muhimu kuifuata kwa kujali rule of law, kujali haki za binadamu.
Kwa upinzani huu wa kupinga kila kitu sitarajii jipya lolote, upinzani wa kukutuhumu fisadi ukihamia upande wao wanakusafisha….

Upinzani wa kuwa mawakili wa wanyonyaji big no. Rwanda inakimbia, Tanzania yenye square kilometers karibia elfu moja inachechemea, tutakumbuka shuka pamekucha.
 
Ukisikia mtu kuwa mjinga, hii ndiyo maana halisi.

Huyu haelewi hata maana ya maendeleo. Hajui kuwa demokrasia ni sehemu ya maendeleo. Hajui kuwa hata katika kanda hii ya Afrika, nchi yenye maendeleo mazuri ya kiuchumi ni Botswana, na Botswana ni kati ya nchi zinazoongoza kwa maendeleo ya demokrasia.

Huyu mjinga hajui kuwa North Korea ilikuwa kwenye hali bora zaidi kuliko South Korea miaka ya 40, lakini udikteta wa North Korea umeifanya hicho hiyo kutopea kwenye umaskini wa kiuchumi ukilinganisha na South Korea yenye demokrasia.

China ilikuwa sawa na Japan, miaka 60, lakini leo Japan ni tajiri maradufu ya China yenye udikteta, tena hali ya China imekuwa afadhali sasa baada ya kuondokana na udikteta ule uliotopea. Leo Japan ni nchi ya 19 katika human development, China ni nchi ya 86, ikizidiwa na hata ya baadhi ya nchi za kiafrika.

Pia linganisha maendeleo ya Hong Kong yenye demokrasia tele na China yenye udikteta. Leo hii Hong Kong na Netherlands ndizo zinazoongoza kuwekeza nchni China.
Mjinga wewe pia hujui kuwa vikwazo mbalimbali vinavyowekwa na wanufaika wa demokrasia ndio hudidimiza Maendeleo ya nchi husika.

Demokrasia iliyo mature ni ushoga, usagaji, matusi ya nguoni hadharani, na ni ushetani.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Sikujua kumbe u mjinga kiasi hicho ndio maana unachezesha tako
 
Ndio quality of thinking ya watu wetu ndio hii?

Yaani kama mwanadamu unataka all your rights and freedoms be confiscated by a group of stupid people called politicians from ccm of course that they will give you free meals and development?

Dont bring authoritarianism here,thats for cows and other mifugo...we are human beings!

You are voting politicians into power kwa ahadi that they will provide free things to you on expense of others then you will have no right to complain when one day they come and take your wealth and distribute to others and for themselves too!
Demokrasia ndiyo inafanya wanasiasa kuahidi vitu free, tena kwa gharama za wengine. Matokeo yake ni kodi na deni la taifa kuongezeka kila siku. Hizi tozo zinaongezeka kila siku ni matokeo ya demokrasia.
 
Badala yake nchi ambayo haina Demokrasia kama Misri ndiyo inaendelea. Ina sera bora za Uchumi nk. Morocco ya kifalme iko mbali kabisa. Hadi tunawaomba watujengee uwanja. Libya ya Gaddafi ilikuwa mbali sana. Hapo hatujazungumzia jinsi South Korea na Singapore zilivyoendelea bila demokrasia. Hatujazungumzia Malaysia ilivyopiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya demokrasia fake.
Wewe inaonekana upo hoi kwenye uelewa.

Unaifahamu South Korea na Singapore au unasimuliwa tu. Wenzio tumeishi kwenye hayo mataifa. Singapore, South Korea, Hong Kong, Malaysia, demokrasia katika nchi hizo ni ya kiwango cha juu kabisa, kinachozikaribia Nordic Countries.
 
Kwa upinzani huu wa kupinga kila kitu sitarajii jipya lolote, upinzani wa kukutuhumu fisadi ukihamia upande wao wanakusafisha….

Upinzani wa kuwa mawakili wa wanyonyaji big no. Rwanda inakimbia, Tanzania yenye square kilometers karibia elfu moja inachechemea, tutakumbuka shuka pamekucha.

Speaking of Rwanda, there is a wisdom saying " it is wearer who knows where the shoe pinches" na waswahili wakasema "kitanda usichokilalia hauwezi kujua kunguni wake".

Wapinzani ni kama kioo ambacho kinakupa reflection ya kuona wapi umekosea, sio wakati wote wataongea mabaya wakati mwingine wanashauri kwa maslahi ya taifa, kuna msemo pia unasema unapoenda kwenye mashindano ambayo unashindana wewe mwenyewe obviously utaibuka wewe ndio mshindi.

Ukitaka accountability and check and balance lazima uache kuona wapinzani wako kama maadui.

#Mama 2025.
 
Wewe inaonekana upo hoi kwenye uelewa.

Unaifahamu South Korea na Singapore au unasimuliwa tu. Wenzio tumeishi kwenye hayo mataifa. Singapore, South Korea, Hong Kong, Malaysia, demokrasia katika nchi hizo ni ya kiwango cha juu kabisa, kinachozikaribia Nordic Countries.
Maendeleo South Korea na Singapore hayajapatikana chini ya demokrasia. Na hao Malaysia walikuwa na Demokrasia jina. Soma historia zao, usiangalie zilivyo sasa.
 
Umeongea ukweli demokrasia inaleta division kama mbinu ambazo mkoloni alitumia kumtawala mtu mweusi
divide and rule
Alikuja Meko hapa katawala miaka 5 tu....
mmeimba nyimbo zote nawashauri bakini na demokrasia yenu

Wewe na mleta mada mmechanganya demokrasia na katiba. Kiasi cha demokrasia tunachostahili wote kimeainishwa katika katiba ambayo ndio hao viongozi wameapa kuilinda na kuitenda!!

Ajabu mnaosema kusiwepo na demokrasia hamsemi kuwe na utawala wa namna gani. Wanajeshi wapindue serikali ya kiraia na ku-suspend katiba? Kusiwe na mahakama? Uongozi wa kiraia upatikane vipi??

Mwishoni mnaonekana maamuma msioweza kusema ni mambo gani hamtaki yasiwepo. Kwani kujenga barabara, viwanda ni mambo ambayo hayakubaliani na demokrasia! Hamtaki wabunge, hamtaki wananchi wachague viongozi? Vipi akipatikana asiyependa maendelea wala demokrasia - mtakuwa hivo mpaka afe??

Pathetic. Low brain capacity!!
 
HII IPO WAZI , HAKUNA NCHI ILIYOPATA MAENDELEO IKIWA CHINI YA DEMOCRACY,
democrasia ni Propaganda za western countries kuingilia mambo ya nchi zisizoendelea ,...( AMINI ).
 
Ni rahisi sana kusema demokrasia haifai,of which ni kweli

Una mbadala wake dunia hii mpaka leo?

HAKUNA!

Hivyo nyamaza kaa kwa kutulia!
Huo ni uzembe. Kwa sababu hakuna mbadala basi tusitoe madhaifu ya mfumo uliopo! Kujua tatizo ni hatua kubwa sana.
 
Speaking of Rwanda, there is a wisdom saying " it is wearer who knows where the shoe pinches" na waswahili wakasema "kitanda usichokilalia hauwezi kujua kunguni wake".

Wapinzani ni kama kioo ambacho kinakupa reflection ya kuona wapi umekosea, sio wakati wote wataongea mabaya wakati mwingine wanashauri kwa maslahi ya taifa, kuna msemo pia unasema unapoenda kwenye mashindano ambayo unashindana wewe mwenyewe obviously utaibuka wewe ndio mshindi.

Ukitaka accountability and check and balance lazima uache kuona wapinzani wako kama maadui.

#Mama 2025.
What exactly are you trying to imply with your quotations? Does that supposed to mean I don’t have rights to comment about anything in regards to Rwanda just because I’m not a Rwandese!

Baki na ideological boundaries za mjerumani, mimi nakupa facts za mwanadamu kiujumla duniani.
 
Hapa watakuja wale wazee wa constitution, watakupinga sana, lkn ukwel ndio huo, nchi kuendelea kwa kutumia udemokrasia ni ngumu, hata hao mabwana zenu waliowaketea hiyo demokrasia wao nchi zao walizijenga kibepar yaan unyonyaji, ukatili na udicteta wa wa hali ya juu, leo hii wameshakuwa developed wanawadanganya naninyi muendekeze demokrsia il mpunguze kasi ya maendeleo.
[emoji117]hakuna nchi iliyoendelea pasipo kutumia udicteta nakaza msimamo haipoooo kamweee, kama unaijua bas ujajua nyuma ya pazia wamepata vip hayo maendeleo.

[emoji117]Demokrasia inanyima uhuru wa kiongoz bora na mwenye msimamo kupata muda mrefu wa kuongoza na kuinyoosha nch

[emoji117]Demokrasia inaendekeza dharau, kejel na uvunjaji wa heshima kwa viongoz wa nchi toka kwa wapumbv wachache wanaotaka uhuru wa kuzungumza na kuutumia vibaya

[emoji117]Udictecta umechafuliwa kwa kupewa sifa mbaya ambazo nyingi ni uongo, mfano mtu kuongoza nchi kwa miaka mingi nje ya elimu za wale waitazo demokrasia huiitwa dicteta, mtu kuminya ama kuzuia vurugu za vyama pinzan pia huitwa dicteta.

[emoji117]Tz bila kuongozwa kikoloni/kifalme itachelewa sana kuyafikia malengo yake, haijalishi hii nchi itaongozwa na kiongoz wa chama gan ama mwenye background gani ya usomi&uongozi, kwa vichwa ngumu vya watz bila fimbo na minyeredi ni ngumu kufanya majukum yao.
 
HII IPO WAZI , HAKUNA NCHI ILIYOPATA MAENDELEO IKIWA CHINI YA DEMOCRACY,
democrasia ni Propaganda za western countries kuingilia mambo ya nchi zisizoendelea ,...( AMINI ).
Kabisa, huwezi jenga uchumi kwa mbinu za kidemokrasia. Demokrasia ni anasa ya matajiri.
 
Africa ndilo bara lenye madikteta wengi na nchi chache za kidemokrasia ila ndilo bara maskini kupita yote pia.
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
 
What exactly are you trying to imply with your quotations? Does that supposed to mean I don’t have rights to comment about anything in regards to Rwanda just because I’m not a Rwandese!

Baki na ideological boundaries za mjerumani, mimi nakupa facts za mwanadamu kiujumla duniani.
Sawa Mkuu.

#Mama 2025.
 
Congo, Africa ya Kati, Sudan, Ethiopia, Guinea, Gabon, Togo, Mali, Zimbabwe na nyingine nyingi zimekaliwa na madikteta tangu zimepata uhuru hadi leo ila ni mafukara wa kutupwa.
demokrasia haina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ila ni chanzo kikubwa ya mambo kwenda pole pole sana! msururu mrefu usio na mantiki
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Kwa hiyo nchi fukara hazihitaji katiba?
 
Mkuu, ni wachache watakao elewa.

Mfano ni north korea. Wakohuru kweli kweli.

Magharibi wanawaona Kama tishio hivo utaona propaganda nyingi utadhani Kule watu hawaishi, tembelea north ujionee jinsi watu wanaishi vizuri kwa amani na huku wakimhusudu kiongozi aliyetokana na asili yao.

Huku kwetu tunahusudu mabeberu ambayo hayajawahi kua na huruma na si.

Yametu enslave,yame tu colonize, yame tuibia railimali zetu, yame tu gawa, yame tu neocolonize, yanatuletea magonjwa--ebola, lakini kwa akili za masalia tunahusudu. Ajabu Sana.
 
Back
Top Bottom