Makuwadi wa soko huria daima wanahubiri kuwa Demokrasia hii ya Kiliberali ndio msingi wa Maendeleo ya kiuchumi. Lakini historia inaonyesha Demokrasia haileti maendeleo ya kiuchumi bali ni zao la Maendeleo ya kiuchumi na huimarisha zaidi Maendeleo.
Na logic yake ni nyepesi tu, ili taifa lolote liendelee kiuchumi, ni lazima lilinde uzalishaji wa ndani, ni lazima liweke kodi kali kwa washindani, ni lazima lidhibiti mipaka yake na uingizwaji wa bidhaa shindani na lazima lihimize ufanya kazi kwa kujitoa. Sasa haya yote huchukua miaka takribani 30 kuyatenda na kufikia Maendeleo hayo. Katika mchakato huo kuna maadui wa nje na ndani, ambao hutumia watu na mbinu mbalimbali kuvuruga, pia yanasababisha uhaba wa bidhaa fulani fulani ambazo kwa mwanzo kuyumbisha ustawi wa jamii. So, haya huweza kutumiwa kuleta chokochoko na kuvuruga michakato hiyo. Ndio hufanya watawala wa wakati husika kuwa wakali na wababe (madikteta). Na hawa huwa ni madikteta wanaojenga jamii (Benevolent dictators). Ndio njia walizopitia Singapore, Korea kusini, China, Vietnam n.k. Baada ya kuendelea kiuchumi, jamii yenyewe automatically inakuwa na mapambano na uhitaji wa Demokrasia hii ya Kiliberali.
Kichotokea Afrika huku, Hii Demokrasia tunayolazimishwa kuitumia, haina lengo la kuleta Maendeleo, bali ni nyenzo ya wezi wa dunia kuiba huku.