Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

bongo mkate hauwezi kuwa chakula kutokana na kazi tunazofanya tunatumia nguvu kuliko akili kwahiyo mkate hautoboi nao kwenye harakati zetu, ndo maana tunapambana na ugali
 
Sisi watu wa mkoa wa Kagera hatupendelei ugali Yani ugali Ni chakula Cha watu wahamiaji ambao hawana mashamba
Me sipendi kabisa ugali
Naweza maliza hata miaka kadhaa sijala ugali
Shana kwamba ukila ugali inakuwa na nguvu Ni uongo
Sisi hatupendelei ugali nguvu na afya njema ipo
Ugali chakula Cha shida
 
Shoppers wana hiyo mikate inauzwa hadi 12000

Huwa najiuliza wanailetaje
Upo mmoja unaitwa street baker una 500g unauzwa Tshs. 21,000 (Brown) na Tshs. 20,000 (white). Shoppers Masaki huwa ikiwekwa tu ktk zile shelves haichukui muda mrefu kumalizika ukilinganisha na ile ya bei nafuu. Sifa kubwa ya huu mkate hauharibiki haraka pia unafaa kwa kutengenezea sandwich. Sandwich nyingi za gharama kubwa zinazotengezwa ktk migahawa na hoteli mbali mbali huu ndio mkate unaotumika sana.
 

Attachments

  • Baker-Street-continues-double-digit-growth-trajectory.jpg
    35.4 KB · Views: 6
Sisi twashindwa wap?
 
Nilishangaa nigeria kuna ugali, tena ugali kwa mlenda, nilijua ni tanzania tu ndio wanakula ugali kumbe hata nchi za afrika magharibi ugali upo. Huenda ugali ukawa ni chakula maarufu duniani.
 
Ukiweza kujizuia mambo matatu utafika mbali;
1. Ugali
2. Pombe
3. Vikao vya hovyo na marafiki wa hovyo.
Mbali ni wapi?mbona kuna watu wapo vzr kiuchumi ,na ugali nyama choma wanapiga,vyombo wanakata na stori za vijiwe wakipata muda wa ziada wanapiga fresh tu,tuache kukariri
 
Hii Ndio mikate sasa
 
Mkuu mkate nchi zingine ni desturi,,
Kwetu huwezi kushindia mkate wakati kuna mihogo, viazi vitamu magimbi, matunda kama yote mboga fungu 500 sasa mkate wa nini?
Vitumbua, chapati , mandazi,vipo
Utasumbukaje na mikate?
Supu mtori, kongoro,mkia vipo mpk kichwa cha mbuzi, mapupu, utumbo vipo.
Utakulaje mikate?
Ukiona mtu anashindia mkate huko unapita ni njaa tu.
Ni chakula cha bei rahisi wanachoweza kukimudu kikawapitisha siku mbili tatu.
Akimega pande moja la boflo akateremshia na cola
Baas mpk kesho.
 
Bufa hukuniambia kama piza kipisi kimoja ni chakula cha usiku πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nilikesha 😩

🀣 🀣 🀣 pole. Now you know.

Jiandae kula mikate asubuhi, mchana na jioni wanabadilisha majina tu; burger, hotdog, pizza, sandwich yote ni mikate tu.
 
wewe shida yako unataka kula mkate ili ufanane na mzungu? au nini? kila watu na tamaduni zao. dunia ya zamani mikate na chapati ndio ilikuwa milo, ndo maana hata mashariki ya kati hata uarabuni na ulaya, ngano ndio wanga namba moja kuliwa kama mlo.
 
Zambia wali wanaweka sukari, Congo wana mikate ina chumvi balaa wana kula soda moja inaitwa slim munene umetoka hiyo mimi nilishindwa kabisa.

Pembeni wana mahungu [emoji3]
 
Kweli mkuu bongo misosi Mingo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…