Kwanza kabisa niseme kwamba,hata uliyoyaandika ni matamanio yako kuona Urusi ikifanya hivyo na Wala hakuna sehemu ambapo Urusi imesema itapeleka makombora ya Nyuklia kwenye mpaka na Finnland and Denmark,Kwahiyo Punguza Mahaba kijana. Putin kasema kwamba,Endapo Finnland na Denmark zikijiunga na NATO,hazitapata faida yoyote ile Bali zitasababisha kusambaratika kwa nchi zao.
Pili,Endapo Urusi akifanya hivyo yaani Ku-INSTALL Nuclear Missiles kwenye Mipaka ya Finland Na Denmark,Basi hiyo itasababisha Nchi Hizo Kukaribisha (HOST) Makombora ya Nyuklia ya Marekani au UK kwenye Mpaka wa Nchi Hizo na Urusi (Kama Finland na Denmark watakuwa wanachama wa NATO). Hili Ni Pigo kubwa kwa Urusi kwasababu Adui wa Urusi si Finland Wala Denmark Bali ni Marekani. Urusi inafanya juu chini kuepuka Hilo.