Nchi ya ovyo sana hii umeme hakuna, maji yanatoka kwa mashaka

Joined
Jul 6, 2022
Posts
70
Reaction score
71
Nashindwa kuelewa kabisa Yani kwamba kuna mgao wa umeme au laaa. Tangu asubuhi huku Msasani hakuna umeme na hakuna taarifa zozote, hiyo haitoshi Jana maji hakuna leo yapo, umeme hakuna. Sasa haya Maji Sijui yanapandaje Kwenye tenki .

Sometimes unashikwa na hasira hakuna shughuli yoyote Maana source zote muhimu hakuna watu wanajiamulia tu kukataa umeme, kuzima Maji Sasa ule mradi wa Kigamboni una maana gani wananchi tushachoka sasa.
 
Ila bila haswaaaaa maji inabadili maisha ya mtu ya kila siku.. ki nguvu na ki akili..

Tunawaombea wanaopitia wakati mgumu huu.. inabidi kuzoea tu.. au???

Kazi iendelee...
 
Ukame,maji ya kupampu hakuna,hata hivyo mipango imetimia huko kigamboni,utapata maji Kama kawaida,ama kwa upande wa umeme vumilia,maana jiwe aliambiwa amalizie project za umeme wa gesi kinyerezi,akakirupukia umeme wa maji rufiji kana kwamba mvua huleta yeye,bwawa hakuna,kinyerezi hakuna,badala ya kutumia midomo yako kulamba nyuchi itumie kuomba mvua mabwawa yajae
 
Unajua kwanini chuma alienda Kwenye maji Kwa sababu gesi ishauzwa Mzee na Serikali inanunua ges kuzalisha umeme na ndio Maana ameenda alikua na nia nzuri ajakosea Wala maana matajorio yalikua kununua umeme point 2. Kwa shilling mia 3 tufout na Sasa Kwa buku
 
Ahahahaha
Serikali imesema ukajifunze matumizi ya H pamoja na irabu 5 ndipo itaacha kukata umeme na maji.
Twende Ulaya tukadai kutawaliwa na Wazungu.
Naunga mkono hoja
Dah ni Kweli nahisi hiyo mikopo wanayotoa wangekuja kujenga wenyewe viongozi Wetu wameshindwa kabisa kitimiza
 
Vyote vipo kwenye mgao shida yako ni nini?
 
Kwa hiyo Kama imeuzwa? Kwa Nini hakuwamalizia bwawa Sasa ili mnunue kwa 300?

Kinachotakiwa Ni matokeo au Nia?
 
Si bora hata nyie Msasani hayo maji mnayapata kwa kuruka siku moja, sisi huku maji hayatoki yapata week 5 sasa 😡😡
 
Naunga mkono hoja yako.
 
Na kunuka jasho kuendelee mpaka dumu muanze kununua kwa shilingi 10000 ndio akili ziwarudi , wanalumumba tena nyie ndio mminywe mpaka maji Muite mma.

Ndorobo wakubwa nyie
 
Hujalazimishwa kuishi tz, kama hapa umeme hakuna na maji nenda Kenya, Somalia au Uganda hata Ulaya. Tusisumbuane we unajua kabisa mito imekauka hata Ruvu imekata unataka umeme na maji kojoa unywe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…