Nchi za Kiarabu muda wa kuishinda Israel ni sasa

Nchi za Kiarabu muda wa kuishinda Israel ni sasa

Viongozi wa nchi za kiislamu wasijitumbukize katika ujinga utakaowagharimu dunia na akhera yao.Kama ni maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu Palestina yapo makumi kadhaa na hayajatekelezwa hata moja.Kinyume chake maazimio hayo yanavunjwa mbele ya macho yao.
Anthony Blinken ameitembelea Israel kuipa pole kutokana na mashambulizi ya Hamas kwenye ardhi zao.Sambamba na yeye ndege za mizigo zimekuwa zikipeleka shehena kubwa za silaha nchini Israel ambayo tangu hapo haina upungufu wa vifaa hivyo.
Sambamba na hilo tena meli kubwa ya kivita na ya kisasa kuliko zote imeshapelekwa jirani kabisa na Gaza na karibu na Israel.Meli hiyo kwa ukubwa wake na vifaa vilivyomo na idadi ya askari wanaokuwemo humo ni sawa na kusema kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani imesogezwa karibu kuisaidia Israel kuimaliza Palestina.
Wakati wa press conference hapo jana kati ya Blinken na Netanyahu kiongozi huyo mkubwa wa Marekani alitaja udugu alionao na Israel.Katika kuomboleza vifo vya raia wa Israel alitokwa na machozi katikati ya hotuba yake.
Baada ya kuondoka hapo imeelezwa ratiba inaonesha ataendelea na ziara kuzitembelea Jordan,Misri na Saudi Arabia.
Nini anakwenda kuwaambia nchi hizo.Huku muda huo huo Israel inaongeza ukatili wake kwa wapalestina ikitaka watu milioni moja na ushei wahame makazi yao katika kipindi cha masaa 24.Pamoja na kwamba haiwezekani kwa muda huo watu idadi hiyo kuhama pia huko wanakoelezwa waende hakuna mazingira ya kuwapokea.Kote ni kifo tu.Watakaoshindwa kuhama watakapouliwa itatolewa sababu kuwa waliambiwa wahame.Kule wanakotakiwa kwenda hakuna nyumba,maji ,chakula na umeme na bado hakuna uhakika kuwa hawatadondoshewa mabomu
Kama ni udugu uliomliza Blinken kwa ndugu zake Israel,jee waislamu na waarabu hawana udugu ulio bora zaidi na wenzao wa Palestina.Waislamu wakizidi kuwa wajinga watamalizwa kabisa.
Sio waislamu sema waarabu kwasababu nchi zile zina hadi wakristo na dini nyingine
 
Huyo sasa hivi lazima arudi kwenye mipaka ya kabla ya 1973.
Hoa wa palestina zaid ya Milion moja wanao hamishwa hujaelewa tu kwamba eneo ndio linachukuliwa moja kwa moja ? Gaza strip baada ya hii vita inakua chini ya milki ya Israel
 
Kwani kuna chi zipi za Kiislam?
Eneo la kijani lote ni nchi za kiislam, hakuna hata moja iliyo tayari kuwapokea waislamu wenzao
20231013_071753.jpg
 
Niliona habari Aljazeera wanamlaumu Abbas kuwa hatoi ushirikiano kwa wenzao wa Ghaza.
Hamasi ni adui zake,
wamemsumbua sana na actually Hamasi wanamuona Abass kama kibaraka wa Israel na Ulaya,

na Abasi na chama chake cha Fatah wanawaona Hamasi kama ni kikwazo kupata mamlaka Kamili ya Palestine, kwasababu wana sura na element za kigaidi kwenye uso wa Dunia
 
hapana,
Lengo la Israel ni kuitokomeza na kuifuta kabisa Hamasi waliojizatiti zaidi Ghaza katika uso wa ardhi ya Palestine.

Mbona West Bank - ukingo wa Magharibi hali iko shwari?
Serikali ya Fatah chini ya Mahamud Abass inaenjoy existence yake with high security, social, political, Technological and economy assistant From Israel.....
Hivi hawa wa Gaza hawawezi kukimbilia kwa ndg zao huko West Bank?
 
Kuishinda Israel ni vigumu!
Walishajaribu katika vita mbali mbali tena wakisaidiwa na Soviet ya zamani kuipiga Israeli, lakini walishindwa! Waliamua kuweka Silaha chini na kutafuta amani na Israel.
Wapalestina na wanachotakiwa kufanya ni kukubali kuitambua Israeli na mipaka ya nchi yake kwanza! Waachane na madai ya kuutaka mji mkuu wa Yerusalem uwe mji wao! Maeneo waliyo nayo ya Ukanda wa Gaza na Ukingo wa mto Jordani unawatosha!
Zaidi ya hapo hawatafaniliwa.
Siyo Israel pekee anayepigana vita na kushinda bali mabwana zake anaowadekea USA na EU ndo humpa kampani ya misaada ya silaha.

Mfano sasahivi Marekani na nchi mbalimbali zinapeleka silaha za kivita Israel ili ipambane na HAMAS.

Israel bila mabwana zake ni wepesi mno kwa HAMAS na wala sio kwa Palestina yote. Size yake ni HAMAS tu.
 
Amekataa? Tupe source ya habari yako mkuu.
SAUTI YA ujerumani umechelewa kidogo but inaendelea, mwisho huwa wanarejea muhtasari wa habari,
subiri BBC, na sauti ya America.

Check aljazeera hadi waandishi wanamlaumu Abass why anakataa kuwahost hata majeruhi tu.

Zaidi sana, madaktari huko Ghaza wanasema wazi wazi kabisa kuwapeleka majeruhi west bank ni kuwakatisha maisha wakiwa wagonjwa ni afaddhalli wabaki Ghaza,wapelekeww huduma tu.....
 
Hivi hawa wa Gaza hawawezi kukimbilia kwa ndg zao huko West Bank?
wamefungiwa kwa maukuta mazito ya zege.Hiyo ingekuwa ni kazi nyepesi.Na sio kwenda west bank bali kuingia Israel na kuingia katika majumba yaliyo karibu yao.
 
H ao ndugu zake Yesu au kawatosa?
Sasa ni lini waisrael walimlilia Yesu awasaidie kwenye vita, wao wanaamini kwenye silaha zao na jeshi lao hatujawahi kusikia wakimuita Yesu wala Yahweh wala Yehova, ila hao wapalestina kila siku wanamlilia Allah ila haendi kuwasaidia ndio maana watu wanahoji yuko wapi huyo Allah wanayemuita kila siku

Halafu miaka yote hiyo ya kuwaponda wakristo na wayahudi, na kujifanya unajua kuchambua na kukosoa vifungu vya Biblia kumbe hujui hata wayahudi wanaamini nini juu ya Yesu, ndio maana unalazimisha kuwanasibisha na wakristo wakati ukristo na uyahudi ni dini mbili tofauti kabisa

Ukae ukijua wayahudi hawaamini kama Yesu ni mwana wa Mungu wao wanaamini yule Messiah aliyetabiriwa kwao bado hajazaliwa, ila atazaliwa siku moja na atakuja kuwakomboa hivyo huyo Yesu wanayemuamini wakristo wao wayahudi hawamtambui kama mkombozi wao kama ulivyomaanisha hapo, wanaamini Torati ya Musa hawalitambui agano jipya na maandiko yao mengi ni tofauti na wakristo
 
Back
Top Bottom