Msisitizo wa Rais kwa siku ya leo ni mshikamano wa nchi yetu, anasema kwenye umoja, kwenye amani tunakwenda vizuri isipokuwa tunachangamoto kwenye mshikamano, hivyo anawaomba Watanzania wote watafakari na kujielekeza katika kujenga mshikamano wa ncho yetu.
Na mimi naungana na Rais katika kuwaomba kwamba namna Pekee ya kuwaenzi Mwalimu Nyerere na Abeid Amani Karume ni katika kuulinda muungano, mahusiano yetu na mshikamano wetu kwa sababu katika kazi yote iliyofanyika katika miaka 62 ya muungano wetu, tutadanganyana kuwa kuna siku mawazo yetu watanzania wote yatafanana, hakuna siku kufikiri kwetu kutafanana lakini tunaweza kukubaliana kutofautiana kwenye mambo mengine halafu tukaenda mbele.
Tunaweza tukakubalaina kwenye maeneo tusiyokubaliaanan tuweze kuvumiliana, kwa sababauu hli ni taifa la watu wanaofikiri Si Taifa la Mawe, mawe ukiyaweka hayafikiri, hayaoni, lakini binadamu wanafikiri na wanaona na kila mtu Mungu amempa kipaji chake cha kufikiri na kuona kwa hiyo ni muhimu tujenge utaratibu wa kuheshimu mawazo ya watu wengine, kuyapa nafasi mawazo ya watu wengine:- Makamu wa Rais, Nchimbi
Pia soma:Hatua saba za muungano wa Tanganyika na Zanzibar