Hiki ndicho alichoongea Gwajima. Nchimbi kakiongea tena. Hapa yeye ameonesha ujasiri na uimara mwenzie alisema ni drama na akawa ana waya waya tu hana mamlaka. Tupate somo kuwafanya watu dhaifu kuwa viongozi.ni hasara kwa Taifa.
View attachment 3429817
Dr. Nchimbi ni Mtanganyika halisi .
Haiwezekani Maslahi ya Tanganyika yakalindwa na Mzanzibari.
Wazanzibari Mil.1.4 hawawezi kutuchagulia Mtu wa kusimamia Rasilimali zetu na maisha yetu .
Huyu Mzanzibari mama yetu mpendwa amechagua kulinda Cheo chake badala ya Rasilimali zetu na uhai wa watu wetu na umoja wetu na mshikamano wetu sisi Watanganyika.
Amechagua kujiweka juu ya dini zetu zote mpaka za asili kwa kujiita chifu mkuu . Lakni pia huyu Mzanzibari mwenye uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Zanzbar ananikumbusha sifa za mtu mhuni kama alivyotafsiri Shekhe kishki kuwa mhuni ni mtu asiye na uraia maalumu . Yaani huyu Rais wetu wa Katiba ni Mzanzibari mwenye asili ya Oman. Yaani hana asili ya Muungano kibaolojia .
Kamwe huyu Rais wetu mpendwa wa watu wachche sana lakni chaguo la katiba ya Kikoloni na kiimla anatumia Ndugu zake wa Zanzibar kujaribu kuiweka Tanganyika chini ya miguu yake.
Nilikua nasikiliza historia ya Warioba halafu nikawa natafakari kuwa Huyu Rais anapata wapi ushauri kama hataki kuwasikiliza Wazee waliopigania uhuru wa nchi hii kwa miaka mingi badala yake anawasikiliza akina Stive Nyerere, Mrisho Mpoki na Nyimbo za kina Diamond za kuhamasisha ukahaba na ushoga badala ya nyimbo za kimapinduzi kama za akina Capt.Komba n.k.
Nikajiuliza pesa za walipa kodi zinatumiwa na wahuni wenye uraia wa nchi Mbili yaani Zanzibar na Tanzania lakni wengine hawana hata asili ya nchi hizi mbili zaidi ya kuvamia Tanganyika kwa ajili ya kujineemesha na kuiacha nchi ikiwa maskini hohe hahe .
Huyu mama yetu mpendwa anatakiwa anitafakari sana .
Nchi hii haimhitaji yeye ndiye anayeihitaji zaidi kwa manufaa yake na uroho wake wa mali na madaraka.
Kama anaona kuwa biashara na Kenya haifai basi aanze kufuta Mkataba wa kupeleka Makaa ya mawe Kenya .
Hapa tutajua kweli ni mzalendo.
Maelefu ya Malori yale yatapaki kwenye mawe au yatakwenda kusafirisha Karafuu kule Zanzibar.
Watanganyika wasikubali kuongeza hata Wiki moja kwa hawa Wazanzibari, kidogo kidogo walianza kuongeza Wizara kwenye Muungano ili kuwapa nafasi nyingi Wazanzibari mil. 1.4 juu ya Watanganyika mil.62+ Hii sio sawa . Ukubwa wa Serikali ya Zanzibar unabebwa na Kodi ya kuumizwa Watanganyika.
Kanchi kadogo wabunge zaidi ya 50 na bado Wawakilishi . Bado Mawaziri .Wakuu wa mikoa ,wakuu wa Wilaya ,mashehia watu wa vikosi maalumu vinavyolonda maslahi ya Watawala wa Zanziba na madaraka yao.
Watu mil. 1.4 ilitosha kabisa kuwa na mikoa mitatu tuu yaani mili Unguja na mmoja pemba . Na wilaya 12 tu .
Lakni pia kanchi ka Zanzibar kalipaswa kuwa na Wabunge kumi tu .
Wanne Pemba na Sita Unguja .
Zanzbar ni nchi ya kisiasa kwa manufaa ya watwala hasa wa CCM na familia zao . Hawa ndio waliojilimbukizia Mali za nchi hii kwa uroho mkubwa sana .
Hawa hawajengi nchi kitaasisi bali kibinfsi maana wana asili ya ubinfsi kama waarabu .Ndio maana hata nyumba za ibada wanajenga kibinafsi ili kupata thawabu binafsi . Yaani mtu anauza hata madawa ya kulevya ili tu ajenge nyumba ya ibada peke yake kwa kudhani tu kuwa atapata thawabu bila kijali umma mkubwa alioudhulumu na kuumiza.
Nchi imekwenda kubaya kwa sababu ya uroho wa madaraka na kujilimbikizia mali .
Tunataka tume huru ili Watanganyika na Wazanzibari washindane kwa hoja namna ya kutumia Rasilimali zetu kwa faida ya Wote hasa Watanganyika walio wengi .
Zanzbar huduma za kijamii zinatolewa kwa gharama nafuu kuliko Tanganyika . Zanzibar hata umeme ni rahisi kuliko Tanganyika wakati umeme unatoka Tanganyika.
Zanzibar kila kitu bei iko chini wakati Tanganika ina rasilimali nyingi na watu wengi na soko kubwa .
Nini kinasababisha Watanganyika watwishwe mzigo mkubwa kwa manufaa ya kakundi kadogo ka Wazanzibari waliojenga mfumo wa ubinafsi kwa Watu wachache kudhibiti wengi kwa vitisho ?
Kwa nini Zanzibar inachukuliwa kama mtoto mlemavu anayetakiwa kubebwa na kubembelezwa badala ya kujitegemea yenyewe kwa usawa .?
Yaani Zanzibar inachukuliwa kama mtoto mchanga anayetakiwa kunyonyeshwa.
Hapa ndipo wanapojitahidi kuimaridha mfumo wa dhulma unaowapa fursa wachche kukwapua mali za umma bila kupigiwa kelele.