King Kong III,
Kwanza awali ya yote ningependa unipatie tafsiri ya beti hizi za Kilingala kama sijakosea.
Baada ya kusema hivo sasa naomba nichangie kuhusu thread hii. Emmanuel Nchimbi alistahili hukumu hii ya kuvuliwa wadhifa wa Uwaziri. From the very beggining Nchimbi hakustahili kuwa Waziri kwa vile hana sifa! Nchimbi ni mojawapo ya mawazir mizigo tangu aanze kuteuliwa kwenye nafasi za Uwaziri. Nakumbuka amewhi kuwa Waziri wa Habari,Michezo na Utamaduni kabla ya kuwa Waziri wa Mambo ya ndani.
Emmanuel Nchimbi alistahili hukumu hii mapema sana. Wengi tunakumbuka jinsi mabavyo alishindwa kusimamia uwajibikaji wa Jeshi la Polisi na UWT katika kushughulikia matukio makubwa kabisa yakiwemo ya MAMBOMU ya Arusha: Olasiti na Soweto. Kwamba mpaka sasa hakuna hata NZI amekamatwa kuhusiana na matukio hayo mabaya katika nchi yetu. lakini pia kuna matukio ya Kuuawa kwa Mwandishi Daudi Mwangosi, Kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka na Mhariri Absolom Kibanda. Mpaka sasa hakuna hata MENDE aliyefikishwa kwa Pilato kuhusiana na unyama huo!
Kama kweli Nchimbi ni Mkristo wa kweli nasema aache unafiki! Hapo alipo hana cha Moyo wa kusamehe wala lolote! Ni huyu huyu Nchimbi aliyeongea Bungeni kwa KIBRI kuhusu Bomu la Soweto lililo lipuliwa kwenye Mkutano wa CHADEMA na kuua watu wanne huku likijeruhi mamia kadhaa. Bwana Nchimbi aliwananga CHADEMA kuwa wao ndiyo waliolipua Bomu hilo kwenye Mkutano wao!!!Haya ni matamshi dhaifu kabisa yaliyowahi kutolewa na mtu mwenye dhamana ya Uwaziri!!!
Watu husema malipo ni hapa hapa duniani. Nchimbi asifikiri zile Damu za Watu kwenye Mkutano wa CDM na Kanisani Olasiti zilikuwa Damu za kuku! Usicheze na Damu ya Mwanadamu mwenzako hata siku moja. Nchimbi kwa ulevi tu wa madaraka aliweza kutamka ulevi wake huo na kusahahu kabisa kuwa Mungu wa Mbinguni, Jehova tunayemwabudu HAZIHAKIWI hata siku moja. Nchimbi ajue kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuharibikiwa. Zile damu za Watanzania wenzetu zilizomwagwa pasi na hatia kuanzia kwa Mwangosi, Olasiti,Soweto na sasa kwenye Operesheni Komesha Ujangili haziwezi kumwacha salama yeye na hao magaidi wenzake kina Nahodha, Kagasheki, Mathayo, IGP Mwema na CDF Mwamnyange!!
Huwezi ukamwaga damu ya mtu na ukabaki salama. Never. Kama Nchimbi ni msomaji wa Biblia basi asome habari za Kaini ndipo atajua maana ya kumwaga Damu ya mtu asiyeka na hatia.
Wasalaamu.