Nchini Tanzania, bullying ni kitu cha kawaida?

kwa bahati mbaya sana, matatizo mengi yanayotusumbua yamekaa sana kisiasa, yani mpaka nguvu ya dola itumike,....
Haya tuwaachie tu waliostaarabika.bila nguvu kubadilika haiwezekani
 
Bullying ni mbaya sana ,,hicho kitu nimejaribu kukifuatilia sana Hususani kwa wenzetu huko Ulaya na marekani.. ndio pale unakuta mtoto anachukua bunduki ya baba yake anaenda nayo shuleni mnakuja kusikiliza breaking niuz baadaye kwamba dent ameua wanafumzi wenzake au mwalimu.
 
Tatizo likishaota miziz linachukua muda na juhudi sana kuling'oa.Nina Imani i
po siku tutaachana na haya.

Imagine shuleni mtoto anakuwa bullied Tena na kundi au darasa zima.maisha huko yatakuwaje?
Mbaya zaidi anaona sio ishu kuripoet na hatua za kuchukua hakuna.
 
Ndiyo hivyo
Ila sie pia wapo wanapigana kisa bullies Kwa jina la utani
 
Bullying ni SILIKA ya viumbe vyote vilivyo hai. Ni namna mojawapo ya kuhakikisha kiumbe kinatambulika miongoni mwa viumbe vingine vilivyopo mahalia. Utasikia kwenye mimea (Plant kingdom)majina kama magugu, invasive species n.k. Hiyo ni mimea inayokaba nafasi au inayovamia maeneo kwa kuishinda ile iliyopo.
Kwa wanyama utasikia kitu kinaitwa vices e.g. kuku kuna "pecking" habits, kwa ng'ombe utasikia "mounting habits" n.k.
Kwa binadamu ndo hiyo inaitwa bullying. Ni kama aina ya Tabia mbovu au mbaya isiyokubalika na jamii au kundi lililopo mahali kwa wakati maalum. e.g. Huko mashuleni esp.boarding sec. schools wavulana wanaoingia kuanza F-one ni lazima wakumbane na jambo hilo kutoka kwa form 2 - hata waalimu wapigie kelele kiasi gani, wakemee haisaidii.
Huko maofisini nako sio haba. Waajiriwa wapya wakifika Ofisini kuripoti kwa mara ya kwanza wakisha ripoti kwa mkuu wa Idara na wakawa-Introduced kwa staff member wengine kinachofuata ni Utelekezwaji. Mtu anaachwa hapo ajijue mwenyewe - atapata wapi nyumba ya kuishi/kulala,chakula n.k. nk.
Matendo au Hali ya kuwa Bullyed around yanajitokeza katika nyanja nyingi sio tu unyanyasaji, udhalilishaji au kufanyiwa vitendo vya kifedhuli, kejeli, kero za kulazimisha n.k. n.k....
Solution: Kama unaweza ni kupuuzia au kama ni lazima kutoa "warning" toa warning ya kiwango cha lami ili iwe ni fundisho na kwa wengine. Usimchekee mtu anayekufanyia bullying kwa kudhamiria. Make or change his/her Perpendicularity into Horizontality absolutely.
Bullying zingine zina madhara makubwa sana. Usikubali kuwa mnyonge.
 
Niliwahi kumuambia mtoto wangu,ni marufuku kunishtakia/kuniambia amepigwa.Mimi nataka nipate kesi zake amembonda mtu siyo yeye kupigwa ila asimchokoze mtu.Akili kichwani mwake.
Are you me or you are me???

Wa kwangu niliwaambia sitaki kesi akipigwa nae ampige tena haswa ili siku nyingine asirudie, iliwasaidia
 
Tushazoea..lakini we mzazi usithubutu kumfanyia hivi mwanao
Wengine wakimdiscourage wewe uwe kinyume nao.hatojali sana
ni kweli ila mzizi wa hii upo mbali sana, yani pata picha mnaenda nje mtania wengine bichwa kubwa, ila baadae mnarudi nyumbani na kuna mmoja ana bichwa kubwa, huyu japo hataniwi na watu wa ndani akili akizipata atakua anasikitika sana kimyakimya
 
Kwa sababu Sisi ni Underdeveloped Kantri. Siku tukitoka kwenye umaskini huu wa mchongo,watu wakiwa wanakula wanashiba na kusaza. Wanapata elimu bora,matibabu yaliyonyooka ndio siku tutakapoanza kufikiria sio tu kuzitungia sheria kali tabia mbovu kama hizo za bullying bali hata haki za wanyama and the like. Kwa sasa bado sana!.
Tukijite kwenye Katiba mpya kwanza!
 
Media pia zina bulliying sana, kuna siku napita pita huko mtandaoni nakuta clip ya Crown Media wamemualika kwenye kipindi huyo mgeni sijui anaitwa somo sijui kungwi, huyo mgeni bila aibu anasema" mtaachwa sana kwa kusingizia mishono" yaani anawasema vibaya wamama waliojifungua kwa mishono kisa wanashindwa kufanya majukumu yao kama wanawake wenginw. Cha kushangaza mtangazaji nae ni mwanamke na yeye anasupport huyo somo anavyowasimanga watu wanaopitia maumivu ya mishono baada ya kujifungua kwa upasuaji.
 
Niliwahi kumuambia mtoto wangu,ni marufuku kunishtakia/kuniambia amepigwa.Mimi nataka nipate kesi zake amembonda mtu siyo yeye kupigwa ila asimchokoze mtu.Akili kichwani mwake.
Kuna siku maisha ya mwanao yatafupishwa kama akiendelea kuufanyia kazi ushauri wako huu hasa kwa dunia hii ambayo watu wana shida ya Afya ya akili. Jaribu kumshauri tofauti.
 
Sasa mtu Kama chivayo unaweza kumwitaje zaidi ya bonge Nyanya SI ndio alivyo

Wakati mwingine upekee wa mtu ndio unakua utambulisho wake mfano toll, short , bonge , ras, kibonge , cheusi , zeruzeru , chiba, kilaza ipo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…