Ndaisaba: Itungwe sheria ya kuzuia watu kunywa pombe muda wa kazi

Ndaisaba: Itungwe sheria ya kuzuia watu kunywa pombe muda wa kazi

Kuna watu bado wana fikra za kijima sana. Kuna mwngne aliwahi shauri mitandao ya kijamii ifungwe wakati wa kazi, mwngne nae aliwahi toa mada hapa akitaka vipindi vya michezo viwe usiku tu ili mda mwngne watu wafanye kazi, yaan unakuta labda mtu yeye ni mlokole hapendi kabisa pombe au hafuatilii michezo, si mpenzi sana wa insta na social media zingine basi anafikiri hayo ndio maisha ambayo kila mtu anatakiwa kuishi.

Ndio maana tunahitaji diversity bungeni bunge liwe na wazee, vijana, wanawake watu wenye mahitaji maalumu, wasomi, wenye elimu za kawaida, wanaharakati, waandishi wa habari lakin pia womehow kuwe na balance kidogo ya vyama hata km sio sana.

Hii itaepusha kundi dogo la watu wenye mtazamo wa aina moja kusababisha nchi yote ikaishi kulingana na mtazamo wao wa maisha.. sisi wa africa hapa ndio tunapokwama ndio maana tunaweza kupata maendeleo ila yakawa si maendeleo endelevu.
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Wee ndiye bure kabisa, kwani wewe una ubongo wa ng'ombe hadi unashindwa kujipangia muda wa kazi na mapumziko?

Jitathimini!
 
Pombe ikatazwe ama ipingwe marufuku kabisa kama tumeweza kupiga marufuku viroba hili nalo linawezekana.
 
Muda wa kazi ndio upi?

Mmoja ni DJ wa music, mwingine ni mwalimu muda wa kazi ndio upi huo?
 
Hii nchi tunahitaji watu wa matabaka mbalimbali, walevi, wavuta sigara, bange n.k. isipokuwa lile kundi la Joe Biden ndo hatulitaki kabisaa tz. Walevi ni resources nzuri kwenye unit's za uchumi wa nchi, kwa kua wanakunywa kwa pesa sio mbaya.
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Wale wanaofanya kazi viwanda vya pombe wahamie majumbani kwenu eti? Muwe mnauliza kwanza mchango wa viwanda vya pombe nchini.
 
Ujue wanaofanya biashara ya pombe wanalipa kodi! Ni mtu kujitambua kuwa unywe mda gani! Kwani moja ya kushushia lunch ni kosa?
 
Mbunge hana taarifa kuwa kuna Sheria ya Vileo ambayo inagusa mambo yote hayo. Inaeleza muda wa kufungua na kufunga baa; aina za kilevi ambacho kinatakiwa kuuzwa katika baa, grocery, maduka na hoteli ; umri unaoruhusiwa kwa mteja kupata kilevi na mengineyo mengi tu yanayohusiana na hayo. Pengine Mbunge angependa kukazia tu hizo sheria kwani yaelekea zimesahauliwa.
 
Stupid thana! mkimaliza mtumpangie na muda wa kunyanduana pia.

au nasema uongo ndugu zangu? 😡😕
 
Ndaisaba hanywi pombe. Atuache walipa kodi wakuu tuendelee kuchangia mshahara na marupurupu yake.

Mwingine muda wake wa kazi ni kuanzia 18.00hrs, so aachwe tu akipigie monde muda anaaona unafaa as long as havunji sheria za Nchi
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Una tabia kama za yule malaika wewe. Pesa wazitafute kwa jasho lao then muwapangie mambo ya kipuuzi
 
Aache mawazo ya kizamani kukalili masaa ni asbh hadi jioni, wengine wanaingia kazini usiku wanatoka asbh anataka hao wanywe pombe saa ngapi? Kwa kupangiana masaa ya kunywa pombe haoni kuwa atakua ameathiri biashara ya wale wanaouza pombe na kulipa kodi?

Anapaswa kufahamu viwanda vya pombe ni kati ya walipaji wakubwa wa kodi, jukumu lake kama mbunge ni kukaa na wapiga kura wake washauriane kunywa responsibly, pia afanye tafiti kwanini wapiga kura wake wanalewa asbh usikute inasababishwa na msongo wa mawazo uliotokana na uongo wa wanasiasa, so inawezekana na yeye ni sehemu ya tatizo.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Nchini Zambia pombe inauzwa kama maji na vijana wa machinga kwenye mabasi na nchi inakwenda.
 
Back
Top Bottom