Ndaisaba: Itungwe sheria ya kuzuia watu kunywa pombe muda wa kazi

Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Kuuza pombe ni kazi pia unataka producers, distributers na sellers wakale wapi? Suluhisho ni kuwekeza kwenye tafiti kwanini watu wanakunywa sana pombe, unaweza kuzuia wasinywe pombe wakahamishia ulevi kwenye kitu kingine, kama walivyoamini kuwa wakifungia viroba vijana wataacha kulewa muda wote matokeo yake wamehamia kwenye chakupima na wanalewa kama kawaida, hii fungia fungia ni uvivu wa kifikiri katika kutafuta solution.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Pombe ikatazwe ama ipingwe marufuku kabisa kama tumeweza kupiga marufuku viroba hili nalo linawezekana.
Unataka watu wote wawe wanapiga swala tano Bwashee!! Dunia haiko hivyo. Na ukitaka iwe hivyo basi vurugu na unafiki vitatawala sana.

Hujashuhudia kumuona Imam/Sheikh/Ustaadh, nk. Akiwa ni Mgigidaji mzuri kwa siri!! Vivyo hivyo kwa Wachungaji/Mapadre/Maaskofu, nk.

Usisahau pia Nchini mwetu, pombe na sigara ni moja ya vyanzo vya uhakika vya mapato ya kuendeshea Serikali yetu. Hivyo ukipiga marufuku, maana yake Serikali itakuwa hoi bin taaban kimapato.
 
Maana yake huyo mbunge ni kuwa viwanda vya tanzania breweries (dar, arusha, mbeya, mwanza), kiwanda cha bia serengeti (dar na moshi) kiwanda cha tanzania distilleries (konyagi), kiwanda cha mega trades (Kiroba org}, Dodoma wine na vingine vingi vifungwe.? Baa zote zifungwe na wahudumu wote na wafanyabiashara wakose kazi.
 
Sitetei pombe ila muda wa kazi ni upi?
Swali makini sana hili
Swali hilo aulizwe huyo bwana ambaye inaelekea hajui kuwa hospital, police, pilots, wanajeshi, wavuvi, tanesco, migodini etc hufanya kazi kwa shift
 
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro amelitaka Bunge kutunga sheria itakayopiga marufuku matumizi ya vileo hadharani.

Ruhoro alitoa kauli hiyo wakati akichangia Mpango wa Serikali jana bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa kunywa pombe hadharani kunasimamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa linashusha ufanisi wa kazi, kutaka watu wasinywe wakati wa kazi.

"Iletwe sheria hapa bungeni itakayopiga marufuku vileo kuuzwa muda wa kazi ili tuipitishe maana haisaidii watu wanashindwa kutimiza majukumu yao wakikimbilia kulewa," amehoji Ruhoro.

Ametaja kundi la vijana kuathirika na kudai wafanyakazi wengi wanatumia saa ya kazi kunywa pombe kwa kuwa muda wa kazi baa huwa zimefunguliwa.

Huyu mbunge amekosa hoja zote za kuwasemea wananchi mpaka anaokoteza hoja ya pombe walengwa wa sheria hiyo ni wapiga KURA wake
 
Angeanza na kutaja muda wa kazi ni saa ngapi mpaka saa ngapi
 
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro amelitaka Bunge kutunga sheria itakayopiga marufuku matumizi ya vileo hadharani.

Ruhoro alitoa kauli hiyo wakati akichangia Mpango wa Serikali jana bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa kunywa pombe hadharani kunasimamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa linashusha ufanisi wa kazi, kutaka watu wasinywe wakati wa kazi.

"Iletwe sheria hapa bungeni itakayopiga marufuku vileo kuuzwa muda wa kazi ili tuipitishe maana haisaidii watu wanashindwa kutimiza majukumu yao wakikimbilia kulewa," amehoji Ruhoro.

Ametaja kundi la vijana kuathirika na kudai wafanyakazi wengi wanatumia saa ya kazi kunywa pombe kwa kuwa muda wa kazi baa huwa zimefunguliwa.
Hawa ni wale ambao hawajui walienda bungeni kufuata nini? Another group kama kina Deo Sanga.
Hivi huyu anajua pombe huliingizia hili Taifa shs ngapi?
Asubiri bajeti ya kikao cha Ccm atajua umuhimu wa pombe kwa Taifa lisilo na wachumi wa kutafuta maeneo ya kodi atajua kwanini walikaa kimya muda wa kunywa pombe baada wa mungu wao kusema ipangiwe muda
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Na pombe ni sera ya wapinzani. Wametuchelewesha sana. Hata vile viwanda vilivyo kuwa vina fugia mbuzi wapinzani walituchelewesha sana
 
Amekosa cha kuchangia huyo mbunge.
Mwisho atasema watu wasitomb@n* hadi Valentine's day!
Asitoshe na akili zake za Kimataga!
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Fungeni viwanda vya bia vyote watu warudi kwenye za asili.
 
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro amelitaka Bunge kutunga sheria itakayopiga marufuku matumizi ya vileo hadharani.

Ruhoro alitoa kauli hiyo wakati akichangia Mpango wa Serikali jana bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa kunywa pombe hadharani kunasimamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa linashusha ufanisi wa kazi, kutaka watu wasinywe wakati wa kazi.

"Iletwe sheria hapa bungeni itakayopiga marufuku vileo kuuzwa muda wa kazi ili tuipitishe maana haisaidii watu wanashindwa kutimiza majukumu yao wakikimbilia kulewa," amehoji Ruhoro.

Ametaja kundi la vijana kuathirika na kudai wafanyakazi wengi wanatumia saa ya kazi kunywa pombe kwa kuwa muda wa kazi baa huwa zimefunguliwa.
Haina mantiki yoyote. Angekuwa sio mnafiki angesema Sheria itungwe Kama Uarabuni na kufunga viwanda vyote vya pombe.Ndio utajua watanzania Kama wasingepata vitu mbadala was hivyo
 
Wakati wowote ni wakati wa pombe. Waacheni watu wajirushe si Watanzania wote ni waajiriwa wa 9 to 5 wengine wako likizo wengine ni wa shift work wengine ni wafanyabiashara na wakulima mtu kauza mzigo wake anaingia bar saa za kazi kwa wengine ili kujipongeza.
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Hela ya kununulia pombe mnagawa bure mpaka unipangie jinsi ya kuitumia?
Kuna mambo mengi ya msingi ya kujadili ktk taifa hili.
 
Angejua kuwa sisi ndio walipakodi wakubwa hapa nchini angeomba tuboreshewe mazingira ya kupiga gambe 24hrs
 
Back
Top Bottom