Ndaisaba: Itungwe sheria ya kuzuia watu kunywa pombe muda wa kazi

Haya mabaki ya Ujamaa yanasumbua sana watu.

Kuna watu watalii wamekuja kutembea, kuna watu wako likizo, kuna watu kazi zao zinahusiana kukutana bar kufanya vikao vya kibiashara, kuna watu kazi zao kupima ubora wa pombe, kwa kunywa wakiwa kazini, sasa wote hao utasema wasinywe pombe wakati wa kazi?
 
Wee ndiye bure kabisa, kwani wewe una ubongo wa ng'ombe hadi unashindwa kujipangia muda wa kazi na mapumziko?

Jitathimini!
Walevi bwana! Yani comments kidogo na matusi juu unatukana, aisee!
 
Kama hii hauli imetoka kwa mbunge Basi tunawabunge wa ajabu Sana Sana na wasiojua wajibu wao.

Moja Kuna leseni ya vileo ambayo inayo masharti lukuki ikiwa ni pamoja na muda uuzaji wa vileo. Je huyo mbunge hajaisoma?

Lakini pili Kuna utata, muda wa kazi ni upi? Kuna wanaoingia 12:00 wanatoka saa babe mchana, wanaoingia saa nane wanatoka saa nne usiku na Kuna wanaoingia usiku wanatoka asubuhi. Je muda wa kazi ni upi?

Tatu vileo na utalii ni sector zinaipatia serikali mapato mengi na fedha za kigeni. Mtalii kaja kupumzika na hayupo kazini, je kwa Nini umpangie muda wa kunywa? Je kipo kutakuwa chanzo mmbadala wa vinywaji?

Nne kupunguza unywaji maana yake ni kupunguza uzalishaji unaoendana na kupunguza nafasi za ajira. Je huoni Kuna kundi kubwa Sana la vijana watakosa ajira kuanzia viwandani Hadi kwenye sehemu za kuuzia vileo?

Tusiongee kabla ya kufanya utafiti
 
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro amelitaka Bunge kutunga sheria itakayopiga marufuku matumizi ya vileo hadharani.

Ruhoro alitoa kauli hiyo wakati akichangia Mpango wa Serikali jana bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa kunywa pombe hadharani kunasimamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa linashusha ufanisi wa kazi, kutaka watu wasinywe wakati wa kazi.

"Iletwe sheria hapa bungeni itakayopiga marufuku vileo kuuzwa muda wa kazi ili tuipitishe maana haisaidii watu wanashindwa kutimiza majukumu yao wakikimbilia kulewa," amehoji Ruhoro.

Ametaja kundi la vijana kuathirika na kudai wafanyakazi wengi wanatumia saa ya kazi kunywa pombe kwa kuwa muda wa kazi baa huwa zimefunguliwa.
Ndo maana masaburi alisema wanatumia ma***ko kufikiria...
 
Mtoa hoja ni kijana au mzee?
Muda wa kazi ni upi!!?? Hawa wawakilishi wetu wanaishi Dunia hii hii tunayoishi sisi au wana dunia yao?
 
Mtu mzima unampangia jinsi ya kuishi wakati humlishi, humvalishi hata kumtafutia tu ajira ili apate hicho kipato umeshindwa...., oohhh wait alafu bado unataka uchukue kodi kwa chochote anachokifanya hata kama ni hizo pombe anazokunywa ?

Hii nchi bana kila mtu Msanii....,
 
Hawa hawa walevi wakigoma kunywa pombe siku 7 uchumi unayumba...mtakusanya nini ktoka TBL na washirika wake? Tuacheni.
 
Mimi kwa akili zangu ndogo ningeshauri watu wanywe pombe wekend tu, kuanzia Ijumaa jioni mpaka jumapili tu, weekdays ni kazi kwenda mbele, tumechelewa sana kwenye hii nchi.
Kutakua na matukio mazito sana weekend's zote kwani itakua fungulia dog
 
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro amelitaka Bunge kutunga sheria itakayopiga marufuku matumizi ya vileo hadharani.

Ruhoro alitoa kauli hiyo wakati akichangia Mpango wa Serikali jana bungeni mjini Dodoma akibainisha kuwa kunywa pombe hadharani kunasimamisha shughuli za maendeleo kwa kuwa linashusha ufanisi wa kazi, kutaka watu wasinywe wakati wa kazi.

"Iletwe sheria hapa bungeni itakayopiga marufuku vileo kuuzwa muda wa kazi ili tuipitishe maana haisaidii watu wanashindwa kutimiza majukumu yao wakikimbilia kulewa," amehoji Ruhoro.

Ametaja kundi la vijana kuathirika na kudai wafanyakazi wengi wanatumia saa ya kazi kunywa pombe kwa kuwa muda wa kazi baa huwa zimefunguliwa.
Ingependeza zaidi iwapo pombe ingetengewa siku maalumu kama week end tuu
 
Dayisabha anazingua. Muda wa kazi ni unaanza na kuisha saa ngapi? Ajue, yeye anavyoingia kazini saa moja na nusu asubuhi, wengine ndo tunakua tunatoka, na Wakati anatoka wengine tunaingia kazini. Asitake sote tuishi kwa ratiba yake.
 
Back
Top Bottom