Ndege aina ya Airbus A220 ya (ATCL) ilifikaje nchini Uholanzi na kukamatwa?

Ndege aina ya Airbus A220 ya (ATCL) ilifikaje nchini Uholanzi na kukamatwa?

Toka January! Wakaja kushtakiwa April.. Kuna miezi 3 katikati
Baada ya kuliona dude litatua kiblah, ndio wakaanza harakati za kudai deni lao ama kukumbushia.. Perfectly timed.. Siku 90 ni kama vile walipewa muda wa kisheria ku clear deni.

Ishu ya kuwa grounded muda wote huo ni mchongo na hata kama tukifanikiwa kulipa deni kuna port charges za grounded feel, hilo dege sijui kama litapona na mshale upi
 
Waliipeleka makusudi ili ikamatwe, kila kitu kimepangwa, hata Tanesco inauzwa pia ndio maana wanakata umeme na maji ili wahalishe.

Walianzia mbali, kwanza walisema Mashirika yalikuwa yanadanganya gawio kwa Serikali halafu wakaja kusema Serikali haitafanya biashara hivyo wameanza kujibinafsisha mali zetu za umma.

Pure evil!
TANESCO atakayeinunua kama atamaliza ujinga wa kukatakata umeme, basi na apewe hata kwa mkopo.
 
Alijuaje inaenda service na inapita huko?
Na yeye alikuwa anasafiri, wakashuka hapo kwa ajili ya kuongeza mafuta. Ile kushuka tu, kutupa macho akastaajabu kuona kitu kimepaki pale, ndo akapiga simu wakaja kuikamata.

Ni sawa na jamaa mmoja aliibiwa gari, baada ya kulitafuta siku nyingi bila mafanikio, siku moja akiwa kwenye daladala lililopitia sheli kujaza mafuta, akaiona gari yake ikiwa inaongeza mafuta. Akaenda kituo cha police kilichokuwa karibu, wakaikamata kiulainiiii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watakuwa wamemtonya wapambe!
Matapeli walioko bongo hapa hapa wanaotaka Pesa bila Shaka ndio watakuwa walimtonya..

Hapa kunatakiwa maelezo ya wahusika,pamoja na kwamba dawa ya Deni Ni kulipa badala ya kuvizia Ila Kuna kamchongo, maza anatakiwa kuwa Mkali..

Unaweza fanya Mambo makubwa na mazuri Ila vitu vidogo Kama hivi ambavyo vinaashiria Mchongo vikaharibu kila kitu.
 
Kampuni feki Kama Richmond inatokea USA inakuja kuchukua uwekezaji kumbe Ni watt wa mjini Mana wachunga ng'ombe hatuwezi jua.
Kama Mauritius inavyosajili kampuni na Seychelles bila complication
Kama hukuishtukia mapema ndio inakula kwako Sasa kwa sababu Hawa huwa smart Sana.

Ni Kama kampuni ya Arab contractor inayozingua kwenye bwawa huko unakuja kujua baadae kwamba Ni kampuni ya kidalali na huwezi vunja Mkataba unaishia kubembelezana..
 
Back
Top Bottom