Ndege aina ya Boeing 737 Max, ni hatari, zimepigwa marufuku nchi nyingi

Ndege aina ya Boeing 737 Max, ni hatari, zimepigwa marufuku nchi nyingi

The Whistleblower

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2022
Posts
247
Reaction score
434
Wanajamvi aina ya hizi ndege zimepigwa marufuku sehemu nyingi sana Duniani baada ya mfululizo wa ajali.

Inadaiwa Boeing 737 Max, ni ndege za kisasa mno lakini zina hitilafu kwenye mifumo yake ya utengenezajji.

Ethiopia hii ndege ilianguka na kuua watu wote, majuzi Marekani hii ndege mlango wake ulifunguka ikiwa angani.

Inadaiwa hizi ndege zimeshusha mno hadhi ya ndege za Boeing Duniani, kwa hiyo zimekuwa grounded na hivyo nyingi kurudishwa kiwandani.

Tanzania leo imepokea ndege hiyo hiyo ya Boeing 737 Max,wanajamvi hii imekaaje?
 
Kweli nimeona CEO Dave Calhoun anaondoka mwaka huu baada ya shutuma kuwa nyingi sana.
 
Wanajamvi aina ya hizi ndege zimepigwa marufuku sehemu nyingi sana Duniani baada ya mfululizo wa ajali...
Boeing is taking a deeper dive. Now ina matatizo mengi na watu wanadai ni tatizo la kuondoa viongozi wahandisi na kuweka watu wanaotanguliza faida.

Whistle blower wake juzi kakutwa amekufa kwenye gari wakati ilikuwa kesho yake akatoe ushahidi dhidi yao. Inasemekana kwamba ameuawa na huenda kutakuwa na uchunguzi na yeye alisema siku mkiambiwa nimejiua mjue wameniua.
 
Msiwe na wasiwasi ikiharibika mafundi wako standby ni swala la kusimama dakika 10 tu wanapiga spana chuma kinaitika watu wanasepa
 
Msiwe na wasiwasi ikiharibika mafundi wako standby ni swala la kusimama dakika 10 tu wanapiga spana chuma kinaitika watu wanasepa
Na ile tuliyoitelekeza nchi ya kigeni vipi, mafundi walishindwa au kwa kuwa ni bombardier
 
Wanajamvi aina ya hizi ndege zimepigwa marufuku sehemu nyingi sana Duniani baada ya mfululizo wa aja...

Mkuu tofautisha 737 Max 8.na 737 Max 9 kabla ya kuanza kuinyanyapaa version isiyohusika na matukio unayoyaongelea.
 
Aliyeagiza hakuwa na maono? Kila siku nazungumzia kuhusu kiongozi mwenye maono. "Visionary leader "
 
Hili swali ni kwenu nyie mamlaka ya usalama wa Ndege zetu, usalama wetu abiria, usalama wa anga letu.
Nisiwachoshe, ukiisikiliza hii video hapa chini, ndege tuliyo nunua bado ni mtihani wa usalama wetu abiria. Wanasema sio salama, ina matatizo mengi sana na inafaa iwe grounded.

Huyu mfanyakazi wa zamani wa Boeing na mpiga filimbi mkubwa anasema kwamba ndege hii ya aina ya max sio salama, ina matatizo makubwa. Serikali njooni huku mtuambie ukweli ni upi kabla hatujachinjwa kama ndugu zetu wa Kule Ethiopia na Indonesia.

Sikilizeni video hii na mutoe majibu ya uhakika kabla hayajatokea ya kutokea maana hawa ngozi nyeupe sisi kwao ni litmus test yao wakati mwingine: Video hii hapa:
View: https://youtu.be/pT4B7oyGBw8?si=3kLm309dbgig8xRO
 
Back
Top Bottom