Ndege aina ya Kware: Kwa mahitaji ya mayai ya Kware, Vifaranga na Kware kwa ajili ya nyama n.k

Ndege aina ya Kware: Kwa mahitaji ya mayai ya Kware, Vifaranga na Kware kwa ajili ya nyama n.k

Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifuatilia kwa kina kidogo sifa nyingi nilizozi sikia kuhusu mayai ya kware, na ninaendelea kutafuta zaidi sababu za kisanyansi kwa sifa hizi kuwa ni mazuri katika mlo kwa ajili ya kusaidia watu wanaokuwa na digestive problem na hata matatizo ya kijinsia ingawa mpaka sasa mimi naamini haipaswi kabisa kuitwa dawa ila chakula kizuri au bora. Na katika kupita huko ndipo moja nilipogundua kuwa katika nutrient 78 za mayai kati ya kware na yale ya kuku nutrient 31 hazimo kabisa kwenye kuku na nyingine zilizobaki ziko sawa na moja ambayo ni vitamin K haipo kwenye kware. Sasa leo nikaona ngoja nione ni kitu gani kilichopo kwenye mayai ya kware ambacho kinasaidia kupunguza uzito na hivyo kufanya mwili ufanye kazi vyema nikagundua kuwa yai la kware lina vitamin nyingi na vile vile good cholestrol nyingi HDL 76 % kwahiyo mtu akitumia inaondoa ile bad cholestrol LDL na hivyo kufanya mwili uwe vizuri zaidi katika kufanya kazi yake, hapa naomba madaktari unisaidie zaidi kufafanusha maana hiyo natoa mada kama a layman.
Adhari mimi ni mfugaji na ninayo mayai nauza ukihitaji vilevile nataka kuilewa kisanyansi zaidi ingawa naona yanaawasaidia watu napenda kupata zaidi sababu za kisanyansi kwanini yanafanya hivyo naomba tujadiliane kistaarabu na kuelimishana
 
Ninayo na nime ku PM bei yake kama unapenda sema tu tray ngapi unataka
 
Ninayo na nime ku PM bei yake kama unapenda sema tu tray ngapi unataka
 
Hivi hayo mayai yanaliwa?

Yanaliwa kama ya kuku tu ila ndio hivyo nutrients zake ninyingi kuliko za kuku kama nilivyotoa kwenye mada kuwa katika nutrient 78 za mayai ya kuku yanakosa nutrients 31 ambazo ziko kwenye kware.
 
Nimekuwa nikipata maswali mengi sana kuhusu tofauti ya mayai ya kware na yale ya kuku sasa katika kutafuta nikasema pamoja na vyanzo vya wataalamu binafsi ningependa kupata vyanzo vilivyo vya kiserekali ambavyo wao hawana upande waliolalia maana hawa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na ajenda zao, Na ndipo nilipopata utafiti wa USDA (United State Department of Agriculture) unaonyesha tofauti za mayai haya kwa kila katika category 78 za nutrients zilizogawanya mayai ya kware yana vitu 31 zaidi ambayo ya kuku hayana kabisa wakati yale ya kuku ya kitu kimoja tu ambacho hakiko kwenye ya kware ambacho naomba nikitaje nacho ni Vitamin K (phylloquinone) na katika hizo 45 vilivyobaki vya kware 42 viko juu na vingine hata mara mbili ya zile za kuku, wakati vya kuku ni 3 vitatu ambayo vimezidi vile vya kware. Angalia link hizo hapo chini kwa number kamili

1. Bofya hapa ikuonyeshe mlinganisho wa mayai ya kware na kuku katika nutrients

2. Bofya hapa uone nutrients za mayai ya kware peeke yake


3. Bofya hapa uone nutrients za mayai ya kuku peeke yake

Naomba niwakilishe nakaribisha maswali au comments au unaweza kutembelea pia www.ulimwenguwakware.blogspot. com ili tuendelee kujifunza zaidi faida ya ndege huyu na manufaa yake katika maisha yetu Ahsanteni na karibuni.
 
Mkuu mimi nimegundua kitu kimoja ni kua mayai ya kwale sasa demand yake imeanza kua kubwa sana,nadhani Watanzania wameanza kulearn umuhimu wa mayai ya kwale kwa mwanadamu japo tumechelewa kulearn ilo!nilikua nane nane Morogoro,mabanda mawili matatu yalikua ya ndege hawa pamoja na mayai yake,lakini wote hawakuweza kumeet demand ya wateja katika kusupply mayai!nimegundua hii ni fursa nyingine inayokuja kwa wafugaji!
 
Kware wanapatikana wapi na wanafugwaje??
 
Kware wanapatikana wapi na wanafugwaje??

Mkuu kwale mara nyingi wafugaji ununua mayai,na kuyaengua kwenye mashine na kupata vifaranga!na utunzwaji wake ni kama kuku,ila hawatoki nje,wanafugiwa ndani
 
Mkuu mimi nimegundua kitu kimoja ni kua mayai ya kwale sasa demand yake imeanza kua kubwa sana,nadhani Watanzania wameanza kulearn umuhimu wa mayai ya kwale kwa mwanadamu japo tumechelewa kulearn ilo!nilikua nane nane Morogoro,mabanda mawili matatu yalikua ya ndege hawa pamoja na mayai yake,lakini wote hawakuweza kumeet demand ya wateja katika kusupply mayai!nimegundua hii ni fursa nyingine inayokuja kwa wafugaji!

Ni kweli mkuu,hata mimi nilichukua tray zangu mbili,ila ni siku za awali kabisa za maonyesho,na tayari nimeyaweka kwa incubator niweze kupata vifaranga vyangu,maana awali nilifuga wachache ili nilisafiri,kurudi nikakukuta wamebaki wawili tu,madogo hawakua makini kuwahudumia!sasa nimeamua kuanza upya!bahati mbaya niliporudi siku ya nane nane nipate hata tray moja ya kula,nikakuta kwenye mabanda yaliyokua na kwale,mayai yote yamekwisha
 
Sawa tuendelee kuwaelimisha ndugu zetu uzuri wake watu wakifahamu manufaa yao kwenye afya zao basi itabidi tukazane kufuga.
 
Mkuu kwale mara nyingi wafugaji ununua mayai,na kuyaengua kwenye mashine na kupata vifaranga!na utunzwaji wake ni kama kuku,ila hawatoki nje,wanafugiwa ndani

Ukiwaachia hawarudi?..
 
wadau naomba kujua bei ya yai moja la kware sokoni ni sh ngapi,,,nasikia mayai yake yana dili sana,,je soko lake liko wapi
 
Bei yake wastani sh.500/- japo wengine wanauza hadi 1, 000/- 'soko lake' ..ina maana unayo unataka kuuza au unayahitaji?
 
Mayai ya Kware ambayo ni mazuri kwa ajili ya afya yako kama chakula bora sasa yanapatikana, kama unahitaji piga 0754-222731. Tshs 20,000 kwa Tray haya ni yale ya kula. Kwa ajili ya kutotolesha yanapatikana kwa Tshs 30,000 kwa tray ya mayai 30. Ahsante na karibu
 
Back
Top Bottom