Ndege iliyonunuliwa na Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner imeondoka nchini Marekani, kutua nchini Oktoba 26 saa nane mchana

Labda walihisi kuna mtu kawafuata nyuma hivyo wakatua Moses lakes kujificha, hawa watu akili zao kama zetu tu za hovyo hovyo.

Au katika majaribio walipata tatizo ndio walikuwa wanalirekebisha hapo Moses Lakes kabla ya kuirudisha kiwandani.

This time italetwa imefungwa kwenye BOX tena usiku, maana kuna kitu wanakiogopa, ila hatufahamu ni nini.Kila siku naona wanaambiwa humu dawa ya deni kulipa, lakini hawasikii.
 
Wale wenzangu na mimi ambao hatuna hata ndoto ya kupanda ndege. Tukutane siku hiyo huenda tukapata lifti bure kutoka kwa mkuu
 

Ndege zimenunuliwa bila idhini ya Bunge. Ni ‘project’ ya Magufuli. Ndio maana wengi hawapendi.

Tanzania ina mambo mengi sana muhimu ya kufanya kimaendeleo kuliko kununua ndege.

Nchi kubwa kama Marekani, Uingereza hawana shirika la ndege la Taifa. Ni ngumu sana kuyaendesha haya mashirika. Utawekeza hela nyingi lakini ultimately yataanguka tu.

RwandAir ya Rwanda kila mwaka inakunywa $50 million kutoka Treasury. Yote ili Kagame aonekane ameleta maendeleo.

We could have built a lot more in Tanzania rather than revive a failing airline. Tungewaachia FastJet na Precision kwa sababu hiyo ni mitaji ya watu binafsi - wakipoteza hatuumi sana.

Kama ni kweli ATCL imefufuka, kwa nini mahesabu yake hayawekwi hadharani? ATCL will die and lose all its aircraft.

But our roads, bridges, airports, power plants, hospitals, schools will remain.

Simple.
 
Mkuu itakuwa siri mpaka lini? Inamaana hii ndege itafanya safari za ndani tu? Mbeya to sumbawanga? Kama serikali inawaza hivi basi hiki kitakuwa kituko Cha mwaka. Maana yake ni kwamba itakapo anza kazi rasmi hawata weka taarifa zake mtandaoni ili wanao book tket waweze kubook?
 
Boss PseudoDar186 Una Point na Hoja ya kujibiwa iwapo mimi Si Msemaji wa Jamhuri na Serikali wala Ikulu.

Ila najua kuna siku Rais alisema kuna Mambo Tanzania yanachelewesha Maendeleo, Mlolongo wa Hatua.
Kuhusu Jamhuri aka Serikali kumiliki ATCL si kweli, nachojua mimi ni Serikali imeipa pesa na kuliwezesha Shirika kufufuka na kujiendesha. Serikali limeinunulia Ndege Shirika, ni kama Shirika limekopa Serikalini.
Kuhusu usiri wa mapato, mimi si msemaji wake.

Ila hata kama yote hampendi, imefikia kweli hata kuombea mabaya Ndege zetu??? !!! Kuombea Ndege zishikwe kweli??? !!!


 
Asante kwa kuweka taarifa saaa
 

Hapa kazi tu.
Watanzania tumechoka kupanda ndege za wenzetu.​
 
Ndege hizi sio zetu, Nilisikia wakati wana kesi kule Afrika Kusini walisema iliyokuwa imekamatwa ni ndege ya RAIS.
Wewe unayesema ndege ZENU unapanda bure au unapewa punguzo ya nauli?

Haiwezekani ndege iwe YENU halafu Ulipie nauli, Imagine kwenu Kuna daladala linapiga misele, Posta- Mwenge -Posta, ukipanda unalipa nauli?
 
Na kwanini waziri anasema waandishi wa habari wakamatwe Kwa kusema kwamba inakuja ndege?
Hili ndilo linaloudhi sana na hawa watu, sijui walizaliwa na kukulia katika mazingira gani hawa.
Kila kitu ni vitisho tuuuu, hawawezi kufanya jambo lolote kwa utulivu?

Taarifa ya ndege kuja ina uhalifu gani hadi kuwatishia kuweka ndani watu. Ukitoa taarifa sahihi kama hiyo wanayotoa sio sahihi inazuia ndege kuja?

Hawa wataacha rekodi mbovu sana katika utawala wao.
Mkandarasi hajatekeleza kazi aliyopewa, pengine kwa sababu zisizokuwa katika uwezo wake, unaamka usingizini unaamru, weka ndani bila hata kutoa maelezo ya uzembe uliofanyika? Na ikibainika kawekwa ndani kwa makosa, yeye hana pa kwenda kutafuta haki yake ya kuvunjiwa heshima! Hii ndio inakuwa sawa katika kutumia madaraka?
 
Moses Lake ni ka mji kadogo ambapo kapo hapo hapo Washington State

Everett [ Seattle} ilipotengenezwa ndege iko west Washington State na Moses Lake iko east Washington State upande wa pili wa Cascade mountains;; huko kuna kiwanja BOEING hukitumia kutest ndege!!!
 
Kwani unadhani ni kweli machafuko yaliyotokea Afrika Kusini ndiyo chanzo cha ndege kuondoa routes zake kule? Wanafahamu ukweli lakini wanajaribu kuuwekea band-aid ili tusiuone, lakini wakiondoa Band-aid licha ya kuona kidonda na uvundo tutauona pia.
Shauri yao, mimi ilimradi ardhi ya Tanzania ipo, naamini nitaishi full life.
 
BOEING 787-8 KUWASILI KUTUA KESHO
▪︎Ni Boeing 787-8 Dreamliner ya pili.
▪︎Kutua Dar es Salaam kesho saa 8:00 mchana.
▪︎Kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Mhe. Rais Magufuli.

#HapaKaziTu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…