Ndege iliyonunuliwa na Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner imeondoka nchini Marekani, kutua nchini Oktoba 26 saa nane mchana

Ndege iliyonunuliwa na Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner imeondoka nchini Marekani, kutua nchini Oktoba 26 saa nane mchana

Hata tetea huwa wanajua kuwa kumekucha lakini jogoo ndiyo mwenye mamlaka ya kutangaza.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Umenichekesha Sana.
 
Kwamba ndege imetoka kiwandani inafikia service? Tumepigwa
Hata kama imetoka kiwandani mkuu, service muhimu. Mbona hata magari yetu tunayoagiza nje huwa tunayafanyia service kabla hatujayaendesha?......Usikute walikuwa wanajaza mafuta pia.
 
Kumbe wanaogopa wanaotuda wasijekulikamata likutua huko makuu kujaza mafuta Hii sababu imekosa viwango vyote vya weledi
Wanaotudai huwa awadili na social media wana njia zao za kupata info
 
Hi itapiga ruti ya wapi China au ulaya itusaidie kuleta maendeleo
 
Ndege mpya iko angani mda huu licha ya baadhi ya viongozi kukanusha. Kumbe wanaogopa wanaotudai wasijekulikamata likutua huko majuu kujaza mafuta. Kesho litatua bongo

View attachment 1244877
View attachment 1244878
View attachment 1244879
View attachment 1244880

▪Ni Boeing 787-8 Dreamliner ya pili.
▪Kutua Dar es Salaam kesho saa 8:00 mchana.
▪Kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Mhe. Rais Magufuli.
View attachment 1244780
DAWA YA DENI NI KULIPA!! HAMNA NAMNA!!
 
Msaada wakuu

MATAGA ni nini au ni nani hawa? Naiona sana lkn sijawahi elewa
 
MIAKA MINNNE TUNA NDEGE IDADI HII MINNE IJAYO TUTAKUWA NA NGAPI ..JUMLISHA WAZEEE WA KUPINGA FC
SIO MAPENZI YA MUNGU KUKIMBILIA NAIRO BI UKAPANDE NDEGE ZA MBALII KAZI INAANZIA HAPAAA
 
Kumbe wanaogopa wanaotuda wasijekulikamata likutua huko makuu kujaza mafuta Hii sababu imekosa viwango vyote vya weledi
rubbish, dreamliner inaondoka mji wowote wa marekani na kutua bongo without refuelling
 
Niko Very serious!
Wewe ndege hizi zikiwepo unafaidikaje? Hupandi bure, hupati discounted fair, na hata faida yake huioni, so unaitaje ndege yenu?

Kunatofauti gani Wakati ndege hazipo na leo zipo? Sio kwamba leo unaweza kutibiwa bure eti kwasababu ndege zipo, na huwezi kupunguziwa gharama kwenye public service yoyote kwa sababu ndege zipo.

Lakini kumbuka wenzako, kama wewe siyo mmoja wao. Wao hupanda BURE, Wanagwiana nyumba za serikali BURE na wakiuziana sio kwa uwazi ni kwa kificho. Wakiugua wanatibiwa bure. Sasa kwanini uziite ndege zetu? Hizi ndege ni ZAO WAO.

Una mawazo finyu sana....kwa uwezo huo wa kufikiria sidhani hata kama unaweza kuikomboa familia yako kwenye umaskini
 
Inashangaza kuona viongozi kuendelea kung'ang'ania biashara yenye hasara mpaka sasa hatujui faida inaingiza kiasi gani ni kama mtu aliyenunua gari ya kutembelea anatoa pesa mfukoni kujaza mafuta ndo mana watu hawataki hata kujiandikisha

Sema wewe ndo haujui...na kama haujui ni bora kuuliza...Nimeamini msemo usemao “ Binadamu wengi wameangamia kwa kukosa maarifa”

Ndege zina faida kubwa ambazo sio za moja kwa moja ( indirect profit)....watalii wengi huwa hawapendi inter connections za ndege hvyo tunapoteza watalii ambao wangeingiza fedha za kigeni kupelekea huduma za afya na miundo mbinu kuwa hafifu.

Ndege ni moja ya njia rahisi na uhakika kuitangaza nchi na vivutio vyake..ukiingia leo kwenye ndege za air Tanzania utakuta magazine zilizo sheheni vivutio vya Tanzania.

Ndege usaidia kufikisha mizigo ya kilimo, ufugaji na bidhaa nyingine kwa haraka na uhakika, huwezi kusafirisha bidhaa za kuharibika haraka kwa meli hvyo ndege usaidia kukudha sector nyngne.

Ndege zinasaidia kusambaza utamaduni wetu wa asili ikiwemo lugha na chakula, Air Tanzania unakuta kiswahili kinapigwa vizur na wageni wanapata kuijua nchi yetu.

Faida ni nyingi sana.
 
MIAKA MINNNE TUNA NDEGE IDADI HII MINNE IJAYO TUTAKUWA NA NGAPI ..JUMLISHA WAZEEE WA KUPINGA FC
SIO MAPENZI YA MUNGU KUKIMBILIA NAIRO BI UKAPANDE NDEGE ZA MBALII KAZI INAANZIA HAPAAA
Vijana hawana ajira
mazao yamekosa masoko
Pembejeo bei ipo juu
Wakulima wa korosho hawajapewa malipo yao
Watu wanatekwa wanauwawa
Democrasia hakuna
Mifuko ya sument bei ipo juu
mwaka wa nne watumishi hawapandishiwi mishahara
Wananchi wanakunywa maji ya madibwi
Biashara zimevunjwa miguu
Viwanda 4000 hewa vimejengwa
Unazani kuna mtu wa kufurahia hizo ndege mtabakia nyinyi wa buku saba kusifia
 
Inakata mawingu kama mamba anavyokata maji.
Way to go JPM, mpaka wasaliti wote wajimalize 💪🏿💪🏿💪🏿
Kwani fedha ni za baba yake yaani kodiyangu na wananchi mwingine Mtu atambie nyie mbona washamba sana
 
Heheheh!

Sasa wale waliotiwa ndani juzi sababu ya kuropoka kuwa dege linakuja nibkwamba walionewa au vile walibeba kazi ya Dr Abbas?
 
Suala sio ndege, hapa hoja zilikuwa kwenye bajeti? Na kama hazikuwemo hauoni ni ubabe wa huyo jiwe kujifanya muhhimili wake umejichimbia chini sana?
Hivi unajua madhara yake, ndege hazileti positive ya moja kwa moja.
Tena ni agharabu sana kwa nchi ya wasanii kama Tanzania ndege zikatuinua.
Anafuja hizi hela kwa kuwa hana uchungu nazo, ila nawambia siku ikifika wote mtamchukia.
Boss Gulwa Hivi mnapata Faida gani kufurahia Ndege yetu na zetu kukamatwa??? !!!
Unajua mimi bado sijafahamu !!!
Kwani ndege haiwezi kuruka moja kwa moja mpaka Tanzania bila kutua kuweka mafuta???? !!!
Tani 40 hivi za mafuta na masaa kama 17 tu hivi ya kuwa angani moja kwa moja.
Kwani Ndege ni za Mh. Rais Magufuli??? !!!
Hauoni na hamuoni faida Watanzania na Wananchi wengi wamepata ajira ??? !!!
Yaani kuanzia Dereva (Pilot) mpaka wahudumu ni WaTanzania, wawakilishi ni wachache sana (Boeing, Kampuni za Engine kama ni tofauti na Boeing).
Wafanyakazi wanaenda Boeing kwa Training na Workshop kibao, ujuzi unaongezeka,
Shirika lilikuwa Nusu Kaputi, limefufuliwa, bado kuna watu hawapendi.
Tubadilike Jomoni.
 
Wanajua ndege sawa na gari, unaweza ikaondoka bila hata booking kujua. Wamegonga mwamba, alisema Mh Sugu, Technology na Number never lie.
Wamesahau kua safari za ndege za abiria haziwezi kufichwa, kila route inayopita lazima iwe recorded.
 
Brain washed
Ndege hizi sio zetu, Nilisikia wakati wana kesi kule Afrika Kusini walisema iliyokuwa imekamatwa ni ndege ya RAIS.
Wewe unayesema ndege ZENU unapanda bure au unapewa punguzo ya nauli?

Haiwezekani ndege iwe YENU halafu Ulipie nauli, Imagine kwenu Kuna daladala linapiga misele, Posta- Mwenge -Posta, ukipanda unalipa nauli?
 
Nyie ndio wapumbavu, ambao bado mnadhani uchumi utakuwa kwa kumiliki ndege.
Umeingia choo cha kike nawaambia.
Mkuu;
Wala usipoteze muda kujenga hoja kwa watu kama hawa!

Kumbuka ukijibishana na mpumbavu kwenye upumbavu wake na wewe utaonekana mpumbavu!

Ni ushauri tu! Samahani kama nitakukwaza!
 
Ndege mpya iko angani mda huu licha ya baadhi ya viongozi kukanusha. Kumbe wanaogopa wanaotudai wasijekulikamata likutua huko majuu kujaza mafuta. Kesho litatua bongo

View attachment 1244877
View attachment 1244878
View attachment 1244879
View attachment 1244880

▪Ni Boeing 787-8 Dreamliner ya pili.
▪Kutua Dar es Salaam kesho saa 8:00 mchana.
▪Kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Mhe. Rais Magufuli.
View attachment 1244780
sasa hivi tanzania mpaka raha lakini nashangaa humu jf kunawatu wana commet za ajabu inaonyesha tu kuwa hawapendi yaani roho inawaumaaaaaaaa na watapata magonja ya moyo mwaka huu tunasonga mbele
 
Back
Top Bottom