Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Ningekuwepo humo ndegeni ningevaa zangu earphone sauti hadi mwisho kabsa. Ningeweka nyimbo ya rose muhando _Nakaza mwenendo nifike mbinguni.
Ningefanya hivyo kwa sababu hata ningepiga makelele ingebadikisha chochote??
Unaongea kirahisi kwasababu akili imetulia huku ardhini. Laiti ungekuwepo huko angani ingekuwa ni full kujamba jamba na kutoa kamasi!
 
View attachment 2306678
Abiria ndani ya ndege ya Kampuni ya Precision, jana waliingiwa na hofu ya usalama wao baada ya injini moja kuzima ikiwa angani.

Ndege hiyo yenye namba PW 467 ikitokea Kahama, ikielekea Dar es Salaam kupitia Mwanza, ilizima injini baada ya dakika 51 kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza.

Hofu ilianza kutokea baada ya abiria mmoja, kijana wa kizungu, kuanza kupiga kelele, akiwaeleza wenzake waliokuwa wameketi jirani, kwamba injini imezima.

Baadaye abiria wengine waliingiwa hofu, huku baadhi wakisali, wakilia na wengine kuonekana wamejiinamia, huku wamefunika nyuso zao.

Baada ya abiria kuonekana 'wakipaniki' ndipo rubani wa ndege hiyo alitangaza kuwepo kwa hitilafu hiyo huku akieleza kwamba hali siyo ya kutisha sana.

"Abiria wetu wapenzi, ndege yetu imepata tatizo la kiufundi, injini moja imezima, lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani, tunapanga kutua katika kiwanja jirani na hapa tulipo," alisema rubani huyo.

Hata hivyo, tulizo la mwana anga huyo halikuleta afueni ya wasiwasi kwa abiria wengi, waliendelea na hofu yao, huku wengine waliokuwa hawajatambua kinachoendelea wakiungana na wengine kusononeka.

Rubani alirejea tena kwa tangazo; "Abiria wetu wapendwa, tunasikitika kwa kilichotokea, nawaomba kuwa watulivu wakati sasa tunajiandaa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Tutatua ndani ya dakika 20."

Baada ya muda huo, ndege hiyo ilitua salama katika uwanja huo na abiria walishangilia. Wengine walipiga kofi, wengine wakipiga kelele za shangwe na wengine wakimshukuru Mungu.

Mmoja wa abiria aliyekuwamo ndani ya ndege hiyo, Simon Mkina, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter na taarifa hiyo kusambaa dunia nzima, huku akipongezwa kwa kutoa taarifa hiyo mapema.

Kwani hakukuwa na maboya
 
mwana JF hebu waza huu uzi ungekuwa unahusu ATCL wachangiaji wangekuwa wanasemaje?
Pamoja na id feki zetu ila members wa jf ni "walewale"
Hapa tungeelekeza matusi yote kwa yule shujaa wa kujivukiza kule kaburini Chato
 
Yes mkuu, binafsi ninafuatilia sana kuhusu vipindi vya Air crash investigation, yule pilot wa Ethiopian Airways alirudi kazini na kuendelea to fly, was sad kwa yule journalist ambaye alipoteza maisha, na wale vijana walioteka Ile ndege hawakuwa kabisa na ABC kuhusu ndege ilivyo na systems zake, kuna tetesi kuwa pilot aliomba atue pale Dar es Salaam int. Airport akanyimwa kibali (but hii ni debate for another time).
Air crash investigation ni bonge la shule kile kipindi.
 
Mkuu unafananisha engine ya ndege na matairi ya gari?
Ndege inayoweza kwenda na engine moja ni ile tu ambayo engine yake imefungwa katikati, kwa maana ya kuigawa hiyo ndege symmetrically. Na ndio maana ndege za engine moja (hasa ndege ndogo), engine hiyo imefungwa katikati mbele. Vinginevyo ingefungwa anywhere lakini katikati ili kuigaga into two halves. Huwezi kupata configuration nyingine.
 
Hivi vitu havijazoeleka sana huku bongo, ndio maana wengiwao hofu inawaingia hahhaa 🤣🤣🤣 ni kama vile mzungu akutane na mende ee bwana eee
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ile height ukiwa kwenye ndege usipopaniki kwa hiyo habari we ni mchawi. Sipendi ndege sinaga namna tu aisee
,
 
Back
Top Bottom