Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Ndege ya Precision yazimika injini ikiwa angani

Kifupi alikuwa anatembelea choki ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Kama ni muvi utasikia; 'Flight nainanaina, we are out of fuel, the plane is flying on vapours'....... hatari mwanawanee.

Ila inakuwaga tamu kwenye muvi tu sio wewe ndiyo uwe ndani laivulaivu wee!

Ila kwa upande mwingine suala la alarm kawaida tu mbona mabasi ya mikoani yanapigaga kale ka spidi gavana ng'ooo ng'ooooo karibu robotatu ya safari halafu kawaida tu!
 
Hizi ndege ndogo nakumbuka niliwahi kukaa pale mbele na pilot, tulikua tunatokea Pemba, ndege ilikua imekwisha kabisa mafuta na ilikua inapiga alarm tukaruka mpaka unguja, hakujaza mafuta, tukaenda nayo mpaka uwanja wa Dar.

Siku hiyo ilikua tete maana jamaa alikua mbishi mno yeye alikua analazimisha kufika dar ndio ajaze mafuta.

Jinga sana yule jamaa.
Kuna ndege inaruka bila ya kuwa na mafuta?
 
Yenye engine moja?
Yes they can but I believe there are other conditions for this to be possible eg pleasant weather meaning no strong wind, heavy clouds
Yes one engine. Under severe weather conditions even two engines can struggle.
 
View attachment 2306678
Abiria ndani ya ndege ya Kampuni ya Precision, jana waliingiwa na hofu ya usalama wao baada ya injini moja kuzima ikiwa angani.

Ndege hiyo yenye namba PW 467 ikitokea Kahama, ikielekea Dar es Salaam kupitia Mwanza, ilizima injini baada ya dakika 51 kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza.

Hofu ilianza kutokea baada ya abiria mmoja, kijana wa kizungu, kuanza kupiga kelele, akiwaeleza wenzake waliokuwa wameketi jirani, kwamba injini imezima.

Baadaye abiria wengine waliingiwa hofu, huku baadhi wakisali, wakilia na wengine kuonekana wamejiinamia, huku wamefunika nyuso zao.

Baada ya abiria kuonekana 'wakipaniki' ndipo rubani wa ndege hiyo alitangaza kuwepo kwa hitilafu hiyo huku akieleza kwamba hali siyo ya kutisha sana.

"Abiria wetu wapenzi, ndege yetu imepata tatizo la kiufundi, injini moja imezima, lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani, tunapanga kutua katika kiwanja jirani na hapa tulipo," alisema rubani huyo.

Hata hivyo, tulizo la mwana anga huyo halikuleta afueni ya wasiwasi kwa abiria wengi, waliendelea na hofu yao, huku wengine waliokuwa hawajatambua kinachoendelea wakiungana na wengine kusononeka.

Rubani alirejea tena kwa tangazo; "Abiria wetu wapendwa, tunasikitika kwa kilichotokea, nawaomba kuwa watulivu wakati sasa tunajiandaa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Tutatua ndani ya dakika 20."

Baada ya muda huo, ndege hiyo ilitua salama katika uwanja huo na abiria walishangilia. Wengine walipiga kofi, wengine wakipiga kelele za shangwe na wengine wakimshukuru Mungu.

Mmoja wa abiria aliyekuwamo ndani ya ndege hiyo, Simon Mkina, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter na taarifa hiyo kusambaa dunia nzima, huku akipongezwa kwa kutoa taarifa hiyo mapema.
Thank God we are safe.
 
Ila ukweli hivi vindege vina fly chini sana kwa MTU mwenye utaalamu anajirusha tu anaogelea angani taaratiiiiiiiibu
 
Au mimi huwa sielewi... ukipanda ndege za Far trip mbona kama kuna wakati mlio wa engine huwa siusikii.. mimi nikajua Pilots huwa anaweza zima Engine m1 kuipumzisha kisha kuiwasha... wakakati ndege ikiwa angani
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ Duh!!!!!
 
Mimi huwa nashangaa vile vindege ambavyo huwa vina pangaboi moja pale mbele tu. Sipati picha Hilo pangaboi likizungua.
Likizingua huwa vinatua hadi juu ya mti ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€. Uzuri wake hata barabarani kanatua.
 
Back
Top Bottom