Tuliwaita mabeberu na majina ya kuwabeza lkn wao bado wanatujali.
Hatimaye dege letu lililokuwa limepigwa pin huko kwa mabeberu hatimaye limefunguliwa.
Asante sana wazungu kwa uwajibikaji.
===
Serikali imesema ndege aina ya Airbus A220 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa nchini Uholanzi imeachiwa na kurejea nchini jana.
“Leo niko hapa kuwapa habari njema, siku chache zilizopita niliwajulisha kuna ndege yetu tulikuwa na kesi nchini Uholanzi ikakamatwa, ilikuwa chini ya mikono ya sheria. Bahati nzuri tumefanya mazungumzo na jambo limekwenda vizuri ndege yetu imerudi jana jioni iko Tanzania,” amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipozungumza na waandishi wa habari leo Julai 8, 2023 mjini Arusha.
Amesema ndege hiyo inaendelea kuandaliwa ili ianze shughuli zake.
“Chuma kimerejea kiko Tanzania, tunaendelea kuimarisha shirika letu, mambo yetu yatakuwa yaanaendelea kuwa mazuri,” amesema Msigwa aliyezungumzia masuala mbalimbali, ikiwamo miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti nchini.
Mwananchi