Ndege ya watalii yapokelewa Uwanja wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)

Ndege ya watalii yapokelewa Uwanja wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)

Kwa waliokaribu na TV tune in TBC 1

======



Ndege ya kwanza ya watalii imewasili nchini ikiwa ni baada ya Rais John Magufuli kuruhusu kuendelea kwa shughuli za utalii nchini baada ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona Tanzania.

Tarehe 20, Mei 2020, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi aliahidi ya kuwa mwishoni mwa Mei ndege ya kwanza ingetua nchini.

Waziri Kigwangala

“Tuna matarajio makubwa kuwa sekta ya utalii na usafiri wa anga itafunguka vizuri kadiri tunavyoelekea”

“Hii ni ndege ya kwanza ya abiria ni ya Ethiopian Airlines, marafiki zetu.”

“Kwa kuanzia Ethiopian Airlines watatua Jumatatu, Alhamis na Jumamosi kwa ndege za abiria. Watatua hapa lakini pia Zanzibar. Kwa sasa wameshusha abiria na mizigo Zanzibar wanashusha na hapa Kilimanjaro, wanaenda Addis na nchi nyingine”

“Kwa siku tano za wiki tutakuwa na ndege zinazotua nchini, lakini zinazotuhusu zaidi watu wa utalii zitatua kwa siku tatu -- Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi -- ambazo purely ni ndege za abiria wote lakini kwa kiasi kikubwa tunatarajia itakuwa ni watalii”

“Dunia inajifunza namna ya kupambana na janga zito kama hili la mlipuko wa Covid 19 bila kufunga shughuli za kiuchumi na maisha ya watu”

Tumejipanga vizuri na tuna uhakika kutakuwa na usalama wa wageni na wahudumu. Tumefanya ziara ya kukagua mifumo na tumejiridhisha kwamba

Naibu Waziri wa Afya, Dr Godwin Mollel

“Ndani ya nchi maambukizi ya Corona kila siku yanapungu, hii ni kumaanisha kuwa kuna mabo yanafanyika”

“Tumehakikisha kuwa miongozo ya Shirika la Afya Duniani na Wizara ya Afya imefuatwa katika kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19”

Meneja Uwanja wa KIA

“Tupo tayari kuipokea kuutangazia dunia kuwa tupo tayari kupokea wageni.”

“Leo tumefurahi kuona tumepokea ndege ya kwanza”

“Kabla ya corona tulikuwa tunapokea abiria wengi sana. Mwaka jana tulikuwa na abiria 28,000 kwa mwezi na hadi kufikia kipindi cha Corona tulikuwa na wastani wa abiria 19,000”

“Tumejipanga vizuri kuwalinda wageni na wageni dhidi ya Covid 19”

Tutakazana sana kuwaaminisha wazungu kwamba tumejipanga kuwalinda dhidi ya corona na hapo ndipo serikali itakapoona umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za corona na kuchukulia mambo kisayansi zaidi kwani hata kama nchi ni ya kwetu ukweli ni kwamba tunashirikiana na watu wengine kutoka mbali na wanapenda kufanya mambo kisayansi.
 
Unaomba msamaha kimtindo! Wazazi wanaingiaje kwenye hoja hii? Wewe wazazi wako ulishawaambia jinsi unavyowakosea wazazi wa wenzako adabu? Kawaeleze Leo kuwa Kuna mzee yupo jf nimemkosea Sana leo kwa kuponzwa na vijisenti vya bando ninavyolipwa na polepole baada ya kuwajibu shit baadhi ya watu!
Vyeo havitafutwi kwa kuwatukana wengine na kujipendekeza Bali kwa maarifa na akili! Wapi musiba????? Uwe na nidhamu!
Mmh an interesting comment...ni kielelezo Cha uelewa wako wa kiwango Cha chini kabisa...ni nani aliyetukana hapa ...hoja yangu ya Kwanza lilikuwa ni swali...kwamba wewe unatakaje...majibu yako yalikuwa ni matusi makubwa..hoja yangu kwa matusi hayo ilikuwa ni kwamba je unaweza ukawaambia wazazi wako ulichoandika hapo...majibu yako ndiyo yanaonyesha pia kiwango Cha chini kabisa Cha uelewa na ni mtu mwenye mtindio wa ubongo ndiye anayeweza kurespond vile..Mara Sijui polepole Mara vijisenti vya bando Mara Sijui kutafuta vyeo..Mara Sijui kuomba msamaha...hivi unaweza kuomba msamaha kwa mwendawazimu? Sidhani..unapata taabu Sana...kwa andiko lako wewe ni mtu uliyeshindikana...huwezi kuelewa chochote zaidi ya matusi...unachukulia JF Kama kichaka Cha kujificha....lakini there is no hiding place in this world...
 
1591105221516.png


Ndege ya shirika la Ndege la Ethiopian Airline imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikitokea Dubai ikiwa imepita takribani miezi mitatu tangu zilipositishwa safari za ndege kuoka nje ya nchi kutokana na tahadhari ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Majira ya saa 11:00 za jioni katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Lilimanjaro (KIA) , Clouds 360 imeshuhudia ndege hiyo iliyobeba watalii ikiwasili katika uwanja huo na kulakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangala aliyekuwa ameongozana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dkt. Godwin Molel .
 
Kwa mustakabali na maslai mapana ya Taifa letu John Pombe Joseph Magufuli, haifai kupewa hata dakika moja, au nafasi nyingine ya kuongoza taifa letu, ametutia aibu Sana , ameturudisha nyuma Kama taifa kwa miaka zaida ya 10, hasara aliyotupa wajukuu zetu hawataweza kulipa
Sisi wengine na ambao tuko wengi JPM ametupeleka miaka 10 mbele
 
Tanzania imebadirika.. vijana wanachapa kazi.
Leo wakati dunia bado haijaamka kuna watalio wawili ambao wanaonekana kwenye picha wamepokelewa na waziri wa utalii.

Hii ji heshima kubwa sana kwa watalii wetu.. na waziri kingwangala ameonyesha kwamba yeye ni mtu wa kazi na si mtu wa cheo na kuletewa chai ofisini.


Big up bro.
IMG_20200602_205228.jpeg
 

Attachments

  • IMG_20200602_204840.jpeg
    IMG_20200602_204840.jpeg
    51 KB · Views: 1
Back
Top Bottom