DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Acha waibe maana tuna ongozwa na vilandege
 
halafu cha ajabu wakiitwa kuhojiwa wathibitishe watalalamika tena wanaonewa!
 
Maasai walituma ushahidi wa ndege kubwa isiyo na alama ikitua na kuruka kutoka Pololeti

View attachment 2473424
Acha kulishwa matango pori nawe ukaleta humu. Pololeti sio Serengeti. Pili, hakuna ndege iliyotua popote kwenye mbuga zetu kwa huo uhuni unaoueleza, mwisho kwa ukubwa wa ndege hiyo haiwezi kutua kwenye maeneo hayo maana hakuna kiwanja cha ukubwa na vigezo vya kuipokea.
 
Chuki na ubaguzi huna kingine
 
Mleta mada ndio ana burden of proof.Ukileta mada hapa JF inayohitaji ushahidi basi wewe uliyeileta hiyo mada ndio unawajibika kuleta ushahidi.
Bila hivyo itakuwa kijiwe cha kila kichaa kuleta upumbavu wake.
Kuna ushahidi kuutoa unakuwa vigumu. Kwanza unaweza kuona hata hiyo video imepatikana kwa kuibiwa. Imepigwa toka vichakani. It's a big risk ambayo Inawezekana amechukua kupata hiyo clip.

Kama ni kweli lazima ulinzi wa pale utakuwa ni mkubwa sana na hawata ruhusu cell phones pale. Hivyo kupata huo ushahidi mnaoutaka haitakuwa ni rahisi kama mnavyofikiria au mnavyotaka.
 
Its insane .hata kama hakuna ukweli ila inaita moyo kuona watanzania sasa wanajua thamani ya mali zao. Jambo la kujiuliza kila mmoja ni kwa nini wananchi wana mashaka Makubwa na hii serikali ? Serikali itupe confidence hatuna shida .something is wrong somewhere
 
Mnaibiwa kitu gani?

Mbona hata Ndege yenyewe haionekani vizuri ili kujua ni Ndege ya wapi?

Ina maana pia hiyo Ndege imetua ndani ya nchi bila mamlaka husika kujua hilo?
Wale twiga na wanyama wengine waliopakiwa wakati ule, mamlaka hazikujua?
 
Mimi nimeuliza swali na wewe unaniuliza swali? au umekurupuka tu bila kusoma comment yangu na kuielewa kwanza?
Kwenye swali langu, unapata majibu..!!!

1. Ili ndege itue uwanja wowote, lazima control towers zijue. Hata inayotua kwa dharula, bado taarifa zinafikishwa sehemu husika. Hivyo mamlaka zinajua kuwa kuna ndege imetua/inatua uwanja fulani.

2. Ndege inapotua, katika taarifa zinazotolewa kwa mamlaka husika, ni sababu za kutua. Hivyo mamlaka zinajua kwanini imetua.

3. Twiga wala haishi airport kwamba ndege imetua ikamkuta hapo. Twiga na wanyama wengine waliopakiwa kwenye ndege, wakiwa HAI huwezi, kuyafanya yote hayo huku wahuska wa uwindaji ETI wawe hawajui. Wapakia mizigo nao lazima wawe wanajua. Unaendaje kupakia mzigo kwenye ndege huku ETI hujui kuwa kuna kupakia mzigo....!! We ukitaka kujua hilo haliwezekani, GONGA TWIGA MBUGANI HUKU UKIWA PEKE YAKO UONE UTAKAVYOKAMATWA NA ASKARI WA WANYAMA PORI..!! Hivyo mamlaka inayohusika na uwindaji inajua kuwa kuna wanyama wamewindwa na kukamatwa wakiwa hai, na wanapelekwa huko wanakopelekwa.
 
Sasa mtu kama wewe hata kuandika lugha yako tu kwa ufasaha huwezi,utaweza kujadili vitu vinavyohitaji akili na maarifa ya utambuzi?
Huu muda unaoutumia kutapika hapa ni vizuri ukautumia kujifundisha kuandika lugha yako kwa ufasaha.
Hakuandika kwa bahati mbaya amekusudia. Ukisoma vizuri utamuelewa.
 
Mimi nimemaanisha ule msemo wa lisemwalo lipo. Na wala sijahitimisha kama ni kweli kwenye hiyo video, wanyama wamebebwa. Maana huko nyuma haya matukio yamewahi kutokea.
 
Eee Mwenye Enzi Mungu amka utusaidie sisi watu wako Watanzania, kumbuka damu za Watanzania ndugu zetu zilizo mwagika kwa ajili ya Africa nzima iwe huru, kumbuka ehh mfalme tulivyo kula chakula cha farasi ili Africa nzima iwe huru, hakuna nchi yeyote Duniani ambayo imefanya hivyo bila maslahi!
Eee Mwenye Enzi Mungu Mfalme wa nchi yetu Tanzania [emoji1241] tunakuita kwa kilio kikuu utusaidie utuokoe katika janga hili kubwa, vilio kwa wanyama wetu, vilio kwa Watanzania!
Eee Mwenye Enzi Mungu tuokoe [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Amka kama ulivyo sikia kilio cha Waisraeli nasi pia utuokoe!
Utuhurumie maana wewe ni mwingi wa rehema na neema!
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Baada ya kuiangalia hii clip wewe unaweza kutueleza nini kinaendelea hapo? Maana hapo imeonekana ndege kubwa porini vumbi na miti na mchukua clip akizungumza aliyoyazungumza. Tumpinge kwa hoja kama yako lakini tusimchallenge sana sababu si mimi wala wewe ambaye tungekuwa na cha ku comment bila ya kuwepo clip hii. Si kila mwananchi anaweza kujua kinachoendelea huko hasa kwa umbali huo. Vipi kama atakuja na Clip ingine ikiwaonesha wanavyopanda hilo dege? Tutasema ni uzushi ama tutafuta kauli zetu? Jambo likiwa linazungumziwa saaana kunakuwa na ukweli ndani yake, Mkuu si mara moja watu wamelizungumzia hili, ni vile tu wanyama hawana uwezo wa kuongea.
NB: Naunga mkono juhudi za Serikali, na kama hii Clip imeletwa hapa kwa agenda ingine ya uzushi basi siungani na mleta thread.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…