Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC

Kwahiyo wao ndio wanakaribishwa? Ni kujisahau tu na mambo ya wanasiasa. We either fall apart or grow together. Ngoja tuone nani atakayepoteza
 
Ndiyo maana ya kwao pia iliyotaka kuwaleta viongozi msibani, anga ilikataa isitue Tz. Wasituletee strain mpya ya kirus 😀
 
Deep state said

Wagen wa kenya walikuja na ajenda ya si i ambayo ni kuambukisa viongozi covid 19
Ndiyo maana ilisitishwa kabla
 
Babu yako kafa juzi. Sababu unaijua? Na kilichowazuia kuja kuzika unakijua. Think critically. Wana lumumba bwana, pumba tupu
Kwaiyo Mkapa uliambiwa anaishi milele, aliyekimbilia kafa Kwa corona ninani? Ndio maana aliwaita Marofa na wapumbavu.
 
Hii imekaeje wadau, kenya wamezuia flights from Tz lkn ndege yao ukiingia mtandao wao bado wanakatisha ticket, au shida ni kutuhujumu tu ili dunia ijue tz sio salama?
 
Hii imekaeje wadau, kenya wamezuia flights from Tz lkn ndege yao ukiingia mtandao wao bado wanakatisha ticket, au shida ni kutuhujumu tu ili dunia ijue tz sio salama?
partner airlines applies
 
Kwaiyo Mkapa uliambiwa anaishi milele, aliyekimbilia kafa Kwa corona ninani? Ndio maana aliwaita Marofa na wapumbavu.
[/QUOTEA

Akili zenu wote ziko sawa na babu yako lofa. Ndiomaana alishindwa kufuata taratibu za kuepuka mikusanyiko hatimae akakutana na tatizo lakushindwa kupumua. Tumeeleza sana taratibu za kujikinga lakini mlivyomalofa hamsikii. mlienda na kijani yenu huko mkapakaa wadudu.
 
Wao wazuie ndege na sisi tuzuie malori ya vyakula toka Tanzania kwenda huko kwao.
Halafu tunaelewana tuu, kidogokidogo
 
Hivi kweli hanuna hata ufa mmoja tunaoeeza kuwafinya ili tuheshimiane,hawa jamaa wanatudharau sana, na Magu aliposema suala la chakula kwenda kwao kipindi kile, waziri wao wa kilimo na chakula alisema wakenya watanunua chakula toka mataifa mengine,sio lazima wanunue Tanzania. Wajinga sana.
 
Back
Top Bottom