Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Wamesema kenya tu. Hawajasema watu. Since kwenda kenya si lazima ndege. Kuna mabasi.. hata miguu.
So hawajazuia raia.

mkuu,nilikua nazungumzia usafiri wa Anga, kwa barabarani sikuwa najua,ahsante kwa ufafanuzi lakini
 
alafu mkuu tuweke tu mambo sawa,Historia sawa,ule umoja uliovunjika miaka ya 70 sisi ndio tulikuwa chanzo, sisi chanzo kikubwa na wakenya chanzo kidogo,Amin hakuwa na kosa
alichokifanya Amin ni kwamba kwa mfano wewe usafiri alafu ukiwa safarini nyumba yako ivaniwe na majambazi ambao walipewa ushirikiano na jirani yako (kenya) so akavunja uhusiano na kenya na aliwategea na Bomu kwenye ndege ya mmoja wa viongozi wao akafa ,na kuhusu Tz ilifadhili uvamizi zaidi ya mara mbili huko Uganda kina museveni walipewa siraha na mafunzo huku ndio maana idd amin akatoa agizo watz na wakenya wote warudi kwao ndani ya masaa 48 na atakayebaki atakuwa kama amekalia moto
Mkuu ungeongea kwa kirefu kidogo ingependeza sana!
 
Mkuu,
Naona wachekeshaji zaidi ni sisi tusiotoa takwimu, tuliamu kuziweka chini ya mvungu halafu tukajitangazia kwamba tuko corona free! Bila ya takwimu ni mjinga peke yake ndie atakaeamini huu upuuzi!
Takwimu kwa ugonjwa upi?
Hata mitaani hauonekani
 
Haya mambo ya twitter kwa Bajabiri kuna haja ya kucopy!? basi jifunze walau kumpa credit jamaa
Jibu ni moja tu,ndege zenyewe kwa ujumla hakuna faida zipo kama mapambo tu na moja ya sababu tumekosa kiongozi katika hili.

Note!!
Li-Sun-Likali jana katimba stendi ya Ifakara akwaambia waliokuwa wapiga kura wake:Jamani samahanini sikujua kama hawa jamaa wako hivi,
Raia mmoja akamwambia hukuwa unawajua?Nilikupa pilipiki na laki 7 zikusaidie kwenye kampeni hukunrudishia hata jero leo unakuja kuzingua
 
Watawala wa Tanzania na wa Kenya watuambie ukweli, siku ya maziko ya mzee wetu tuliona taarifa kwenye mitandao na vyombo rasmi vya habari kuwa ndege iliyokuwa na wajumbe kutoka Kenya waliokuwa wanakuja Tanzania kushiriki nasi kumzika mzee wetu ilizuiwa kutua uwanja wa JNIA na kutakiwa kurudi Nairobi, Kenya.

Na baada ya siku moja tuliona balozi wa Kenya akikanusha na kutoa taarifa kuwa ndege iliyokuwa na hitilafu ndio maana ikatakiwa kurudi Nairobi.

Kabla Mambo hayajakaa sawa tukiwa bado tunajiuliza nini kilitokea na kutafakari kauli ya balozi eti ndege ilikuwa na hitilafu kwa nini irudi Nairobi isitue viwanja vya karibu au hata KIA?

Gafla tunaona Kenya wanataja nchi zinazo takiwa kurusha ndege zao katika anga ya Kenya sisi majirani zao hatupo.
Ndani ya muda mfupi tunaona wabogo wanajibu mapigo kwa kufunga anga yetu kwa shirika la ndege la Kenya.

Nataka kujua kwenye hili zuio la ndege inahusu mashirika ya ndege ya haya mataifa tu kwa maana ya Air Tanzania na Kenya Airways? Au inahusu ndege yeyote itakayotua Kenya haitaruhusiwa kuja Tanzania au ndege yeyote itakayo tua Tanzania haitaruhusiwa kutua Kenya? Umoja wa nchi za Afrika Mashariki unaelekea kufa na dalili ndio hizi, kwa Mara hii Tanzania ndio tutalaumiwa kuvunja umoja wetu uliopiganiwa na kurejeshwa na mzee wetu mkapa baada ya uliokuwa Umoja wa Afrika Mashariki kuvunjika mwaka 1977.
Wao walikuwa wamezuia ndege zetu kuingia nchini kwako, ilihali wao ndege zao walipanga kuanzia leo zianze kuja hapa kwetu,

Tena ndio nchi pekee EA wamepanga kurusha ndege mara nyingi kuliko nchi nyingine yeyote.

Hawa jamaa sijui wanafikiriaga vipi
IMG_6vtrtv.jpeg
 
Watawala wa Tanzania na wa Kenya watuambie ukweli, siku ya maziko ya mzee wetu tuliona taarifa kwenye mitandao na vyombo rasmi vya habari kuwa ndege iliyokuwa na wajumbe kutoka Kenya waliokuwa wanakuja Tanzania kushiriki nasi kumzika mzee wetu ilizuiwa kutua uwanja wa JNIA na kutakiwa kurudi Nairobi, Kenya.

Na baada ya siku moja tuliona balozi wa Kenya akikanusha na kutoa taarifa kuwa ndege iliyokuwa na hitilafu ndio maana ikatakiwa kurudi Nairobi.

Kabla Mambo hayajakaa sawa tukiwa bado tunajiuliza nini kilitokea na kutafakari kauli ya balozi eti ndege ilikuwa na hitilafu kwa nini irudi Nairobi isitue viwanja vya karibu au hata KIA?

Gafla tunaona Kenya wanataja nchi zinazo takiwa kurusha ndege zao katika anga ya Kenya sisi majirani zao hatupo.
Ndani ya muda mfupi tunaona wabogo wanajibu mapigo kwa kufunga anga yetu kwa shirika la ndege la Kenya.

Nataka kujua kwenye hili zuio la ndege inahusu mashirika ya ndege ya haya mataifa tu kwa maana ya Air Tanzania na Kenya Airways? Au inahusu ndege yeyote itakayotua Kenya haitaruhusiwa kuja Tanzania au ndege yeyote itakayo tua Tanzania haitaruhusiwa kutua Kenya? Umoja wa nchi za Afrika Mashariki unaelekea kufa na dalili ndio hizi, kwa Mara hii Tanzania ndio tutalaumiwa kuvunja umoja wetu uliopiganiwa na kurejeshwa na mzee wetu mkapa baada ya uliokuwa Umoja wa Afrika Mashariki kuvunjika mwaka 1977.
Hata Malawi wameizuia KQ kwenda kwao. Sasa wewe endelea na kufikiria EAU badala ya kufikiria maslahi ya nchi yako zaidi.
 
Inaonekana hata kutumia ndege hasa international flights hujawahi au mara chache sana umesafiri nje ya TZ. Unaposema direct flights from where to where? Hapa TZ kuna direct flights from Dar to Dubai, Amsterdam etc. ambako ndiko kwenye hub ya kwenda US na sehemu nyingine duniani. Sasa unaposema eti lazima uende Nairobi wakati kuna mashirika mengi tu yanayokuja Dar ya direct flights to those hubs mentioned above yakiwemo KLM, etc.
Umesoma nilichoandika na kuelewa?! Hivi nimesema hakuna direct flights au nimesema hatuna direct flights nyingi compared to JKIA? Nimesema ni LAZIMA uende Nairobi au nimesema kwenda NCHI NYINGI tu mtu unalazimika kupitia Nairobi?!

Halafu angalia unavyojichanganya! Ukishatoka Dar kwa lengo la kwenda US, lakini ukapitia Dubai na hapo ukabadili ndege to US; hiyo haiitwi direct flight!! Ni kawaida sana unakuta mtu unaondoka Dar na ndege ya Qatar Airways, halafu ukifika Dubai au Doha, unabadilisha ndege na kuchukua nyingine to final destination!

Hata kama hiyo ndege nyingine ni ya Qatar, hiyo bado huwezi kuita direct flight!!
 
Mwenye uzi hapo juu nenda Kenya utuachie nch yetu ili tujue hatuna Mtu sisi wafia Nchi tuendelee na mapambano ya ujenzi wa Taifa letu Tanzania aslani hatuna mbadala.
 
KWANZA ONDOA UPUMBAVU WAKO WA TANGZAZO LAKO LA KIINGEREZA HAPA .SISI TUMEONA NA KUSIKIA KUTOKA KWENYE VYOMBO VYAO WENYEWE VYA HABARI KUHUSU NDEGE ZA TANZANIA KUTORUHUSIWA KUTUA KENYA. PILI, WEWE PEKE YAKO UNAWEZA UKAJUA HIYO LUGHA LAKINI USIDHANI WATANZANIA WENGINE WOTE WALIOBAKI NI WAJINGA,WANAWEZA KUYATAZAMA MAMBO NA KUSOMA KATIKATI YA MISTARI.
MASUALA YENYE MITIZAMO YA KIUCHUMI MARA KWA MARA HUWA NI MAGUMU KUYAELEWA NA HASA KWA WAJINGA WACHACHE AMBAO WANADHANI KUONGEA KIINGEREZA PEKE YAKE NDIYO UNAWEZA UKAENDELEA.HUU NI UJINGA WA KASUMBA TULIORITHISHWA NA WAKOLONI WETU AMBAO HATA BAADA YA KUONDOKA KWA ZAIDI YA MIAKA 50 ILIYOPITA BADO TUNAABUDU LUGHA YAO.
MWISHO, TUNAIMANI KUBWA KABISA KWAMBA JAMBO HILI LITATATULIWA NA NCHI HUSIKA KWA MAELEWANO NA KWA KUHESHIMIANA.
 
Wewe na mtoa mada wewe ndie umeonyesha kua ni mpumbavu. Herufi kubwa za nini? Unapayuka na kupiga kelele.
 
Mwenye uzi hapo juu nenda Kenya utuachie nch yetu ili tujue hatuna Mtu sisi wafia Nchi tuendelee na mapambano ya ujenzi wa Taifa letu Tanzania aslani hatuna mbadala.
Wewe mfia nchi au mfia utopolo wa watawala
 
Back
Top Bottom