Ndege zashindwa kutua KIA kisa taa za runway kutofanya kazi, KLM yaenda kutua Entebbe

Ndege zashindwa kutua KIA kisa taa za runway kutofanya kazi, KLM yaenda kutua Entebbe

Architect E.M

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
1,222
Reaction score
1,425
Wanabodi, hii imetokea jioni hii, mpaka sasa ndege zimeshindwa kutua KIA, chanzo kikiwa kutokufanya kazi kwa taa za runway.

Precison iliyotoka Dar jioni hii imekua re routed to Nairobi as we speak, wameambiwa matengenezo might take up to 5 hours.

Wahusika changamkeni kurekebisha tatizo.

=======

UPDATES;

=======

Alipotafutwa kutoa ufafanuzi juu ya taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendeshaji na Uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wa Kia (KADCO), Christine Mwakatobe amesema amesikiliza swali kisha akasema yupo kikaoni na kukata simu.

Hata alipotafutwa baadaye kwa kupigiwa simu na kutumiwa ujumbe wa maandishi (SMS) hakutoa ushirikiano.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amethibitisha Taa za njia ya ndege zilizima kuanzia saa moja Usiku hadi saa tano Usiku kutokana na Mvua nyingi zinazoendelea kunyesha na kuathiri miundombinu.

Ndege iliyokuwa itue muda huo, ililazimika kwenda kutua Entebbe Nchini Uganda.

Hakuna abiria hata mmoja aliyetelekezwa na na Wote watarudi Tanzania.

Ameongeza Uwanja wa KIA baada ya kufanyiwa Marekebisho, kuanzia jana Usiku saa tano na nusu hadi sasa Uwanja unafanya kazi kama kawaida.

IMG-20230406-WA0013(1).jpg
IMG-20230406-WA0012(1).jpg
IMG-20230406-WA0010.jpg
IMG-20230406-WA0011.jpg
 
Wanabodi, hii imetokea jioni hii, mpaka sasa ndege zimeshindwa kutua KIA, chanzo kikiwa kutokufanya kazi kwa taa za runway.

Precison iliyotoka dar jioni hii imekua re routed to Nairobi as we speak, wameambiwa matengenezo might take up to 5 hours.

Wahusika changamkeni kurekebisha tatizo.
Ninekumbuka ile ndege iliyo angukia ziwani kule kagera
 
1680801862061.png

Ndege ya KLM kutoka Amsterdam imeshindwa kutua uwanja wa ndege wa KIA masaa machache yaliyopita na kusababisha watalii na watu wengine karibu 150 kushindwa kuingia nchini.

Ndege hiyo ililazimika kwenda kutua Entebbe ambako taa zilikuwa zinaangaza kwa manjonjo yote. Pamoja na watu wazima wengi ndege hiyo imebeba wamama wajawazito, watoto na wazee ambao sasa wanahangaika kutafuta usafiri wa haraka.

Haieleweki tatizo ni taa au umeme au upepo. Kuna watu wengine wamesikika wakilitaja Jina la yule Marehemu Mpendwa, wakionesha kusikitishwa na Tanzania kuzidiwa na umeme wa Jinja.
 
Ujinga mtupu, tatizo la kukatika kwa umeme lilianza miezi michache kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2020. Tuna kumbukumbu ya kutosha kuhusu tatizo hilo. Hao waliomtaja labda ni sukuma gang. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
 
Wakitaka kujifariji wanamtaja.Wakishambuliwa wanasema msimtaje mfu,Kiafrika haipendezi.Vimbwenerehi wana vituko sana.😂
 
Back
Top Bottom