Wakuu,
Naona CHADEMA leo wanataka kutulaza saa tisa usiku

.Maana ndio kwanza wapo kwenye zoezi la kuhakiki wajumbe, mara wamesema sijui kuna kanda ya Rukwahaikuwepo kwenye orodha, hapo inabidi wajadili tena ili naowahakikiwe. Kupoteza muda tu.
Wakimaliza kuhakiki wajumbe, wanatakiwa kumchagua mwenyekitu wa uchaguzi atakayeongoza zoezi hilo, halafu wagombea waitwe kujinadi! Wamalize wote kujinadi na kujibu maswali ndio waanze kupiga kura. Na hapo bado hawajaenda kura!
Hii haiwezi kuwa bahati mbaya, mambo yafanyike usiku mwingi ili wafanye umafia! Sisi vimbelembele ndio hatutali hadi kieleweke! Tutabaki macho hata tukiwa mazombi 😒😒