Hakuna kazi ngumu Kwa mgalatia kama kuutetea ukristo Kwa kutumia maandiko
Ona ulivyo andika garazeti hapo kitu Chochote Cha uongo lazima uzunguke sana Ili kukielezea
BIBILIA IMECHAKACHULIWA
Kama wewe unapinga kuwa Taurati na Injili hazijachakachuliwa basi unapingana na Bibilia maana Bibilia linakubali kuwa hivyo vitabu vimechakachuliwa
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Kutia mikono maana yake Nini?
Kutunga maana yake Nini?
UKRISTO ULIANZISHWA NA PAULO
Matendo ya Mitume 11:26
hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
YESU WANAFUNZI WAKE ALIWAACHA WAKIFANYA IBADA NDANI YA SINAGOGI
Hadi siku Yesu anapaa mbinguni kulikuwa hakuna dini inayoitwa ukristo Wala jengo linaloitwa kanisa Wala mtu anayeitwa Padre au papa
Yesu aliwaacha wanafunzi wake wakiabudu ndani ya masinagogi na akauzuniswa na yatakayo tokea Baada ya yeye kuondoka Yani wanafunzi wake kutengwa na masinagogi
Na hiyo kazi alikuja kuifanya Paulo akiwa ametumwa na warumi
Yohana 16:1
Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
Yohana 16:2
Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
Yohana 16:3
Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
IBADA YA KUSUJUDU YESU NA WANAFUNZI WAKE
Mathayo 26:39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Hapo Yesu anaongea hayo Maneno huku paji lake la uso likiwa limegusa aridhi
Lakipia pia Yesu anajua na amefundisha kuwa Mungu lazima asujudiwe
Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
YESU AMEFUNDISHA MUNGU NI MMOJA TU NA YEYE AMETUMWA NA HUYO MUNGU MMOJA
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Kwanini nyinyi wagalatia mkianza ibada mnasema Kwa jina la baba mwana na roho mtakatifu kama sio kuabudu Miungu 3
KUTAWADHA KABLA YA IBADA
Manabii wote unaowajua wewe walitawadha kabla ya kufanya ibada hilo ni agizo la Mungu
Nyinyi wagalatia hamtawadhi Kwa sababu dini yenyewe mmeletewa na wapagani
NABII MUHAMMAD NDANI YA BIBILIA
Kumbukumbu la Torati 33:2
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
Andiko linasema bwana alitoka Sinai
Mlima Sinai kapewa utume nabii Musa
Kisha akaenda Seiri
Mlima Seiri upo katika eneo la Yuda kapewa utume Yesu
Alipotoka Seiri bwana akaangaza mlima wa Parani
Mlima Parani upo Saudi Arabia kapewa utume mtume Muhammad
Ila Kwa sababu wewe ni kafiri na kazi ya kafiri ni kipinga maandiko ya Mungu
Labda useme Kwa Nini bwana alipo toka nchi ya Yuda akaangaza Saudi Arabia kulikuwa na Nini huko Saudi Arabia?