Ndoa ina raha yake bwana asikwambie mtu, japo maudhi yapo ila sio mengi kama mazuri

Ndoa ina raha yake bwana asikwambie mtu, japo maudhi yapo ila sio mengi kama mazuri

No marriage is perfect, those celebrating 30,40,50 years of togetherness, they are celebrating forgiveness, tolerance, ignoring the husband's stupidity, overlooking the wife's misbehavior, etc. *Money does not determine a better marriage but character and loyalty do. ♥️👌
 
Uzi tayari
Uzi huu umekaa kimtego-mtego kweli. Unatuonesha Upande mmoja wa maisha ndoani ili waboboezi wakuambie yale ya Upande wa pili. Bro; ndoa haina Formula(Kanuni) Wapo wanandoa walioumizwa mno na wenza wao hata umauti ukawashukia.
Neno raha linategemea yule anayelitumia anakusudia ujumbe gani.
e.g. Kama wewe ni mtu wa kupenda kuninihino sana, maisha ya ndoa yanaweza kuwa ni msaada kwako ili uepuke uwezekano wa kukanyaga miwaya au maswala ya ugoni. Kwa hiyo, hilo laweza kuwa ni raha kwako.
 
No marriage is perfect, those celebrating 30,40,50 years of togetherness, they are celebrating forgiveness, tolerance, ignoring the husband's stupidity, overlooking the wife's misbehavior, etc. *Money does not determine a better marriage but character and loyalty do. ♥️👌
But with red lines.(limits).
 
Faida ni nyingi Kuliko hasara.

Imagine nikisharudi Home nimechoka na kazi, nimerudi na Posho kadhaa kutoka kwa boss.

Narudi nyumbani nakutana na haya;
1. Mke mzuri, mcheshi
2. Watoto wangu watatu wazuriz
, wasafi. Wanan'gaa
3. Nyumba ina ng'aa ndani na nje
4. Kitanda kimetandikwa kama cha Mfalme fulani hivi wa Uarabuni.
5. Narudi nikiwa na furaha sana, siri mtaani kwani chakula bora kinanisubiri nyumbani
6. Watoto wangu wanaonipenda wananigombania kila mmoja anataka nimpakate yeye

7. Baada ya kula naingia JFs
8. Napiga viwili vya heshima napumzika
9. Siku inaendelea kuzunga, life goes on.

Ndoa ina raha kubwa sana.
Kuna mwamba mmoja akiusoma huu muandiko atahisi kama kachelewa sana kuvuta jiko. Na mie namshauri hivi bora aendelee kuchelewa
 
Faida ni nyingi Kuliko hasara.

Imagine nikisharudi Home nimechoka na kazi, nimerudi na Posho kadhaa kutoka kwa boss.

Narudi nyumbani nakutana na haya;
1. Mke mzuri, mcheshi
2. Watoto wangu watatu wazuriz
, wasafi. Wanan'gaa
3. Nyumba ina ng'aa ndani na nje
4. Kitanda kimetandikwa kama cha Mfalme fulani hivi wa Uarabuni.
5. Narudi nikiwa na furaha sana, siri mtaani kwani chakula bora kinanisubiri nyumbani
6. Watoto wangu wanaonipenda wananigombania kila mmoja anataka nimpakate yeye

7. Baada ya kula naingia JFs
8. Napiga viwili vya heshima napumzika
9. Siku inaendelea kuzunga, life goes on.

Ndoa ina raha kubwa sana.
Pointi hapo ni moja, kama unapenda watoto, ndoa ndio mahala pake.

Sisi ambao tuna mtoto mmoja tu na yuko Marekani, na hatuna mpango wa kuwa na mtoto mwingine, ndoa ni scam tu.
 
Ndoa mpya hii 😂 😂 😂 😂
Nipo kwenye basi sasa hivi. Mdada mzuri natural kakimbia mume wake kisa alikuwa anatuma sms Hajibu anapiga simu hapokei. Wakati huo alikuwa yupo mbali na yeye. Na kamwacha ana mtoto mmoja na ana mimba. Baadaye mdada akasema tuachane kila mmoja aendelee na maisha yake. Binti akaondoka na mimba yake. Akajifungua akarudi. Akaanza kuomba msamaha jamaa kagoma kata kata. Kaomba mshenga, wazazi wa mshikaji lakini kagoma. Baada ya hapo dada kaamua kuondoka hata anakokwenda hajui. Ila kamwachia watoto wawili. Mmoja ana miaka 3 na mwingine ana mwaka 1. Analia basi zima. Ikambidi nianze kujua kuna shida.

But kwa kiasi kikubwa naona ni utoto unavunja hii ndoa. Lakini ndoa zinahitaji uvumilivu. Sasa kajua mmewe ana mwanamke mwingine. Ila anatoka na ataishia kudate na mme wa mtu.

Wanadamu wanadamu tujifunze hakuna kitu kipya duniani. Hakuna mtu mkamilifu. Mnatakiwa kuvumiliana. Watoto mnawaleta duniani wanapata shida kisa uadui wenu baada ya ndoa.

Tuache kusikiliza familia zetu sana tunazotoka ndo chanzo cha mifarakano. Ukiwa na upendo zaidi nyumbani kuliko familia unayojenga huwezi jenga nyumba yako. Nyumba unayoipenda sana ilijengwa na baba na mama yako. Je jiulize wewe watoto wako utawarithisha nini? Tujifunze kitu hapa siyo mwandishi mzuri ila naamini nitataeleweka.
Binadamu tunatofautiana.

Kuna mtu vijimambo vya kwenye ndoa vinampa furaha, mimi vinanikera tu.

Mara uulizwe unachati na nani, eti kufika nyumbani mwisho saa mbili, mara uambiwe leo hakuna kwenda kuangalia mpira..

Mara mtu kanuna siku nzima eti shoga ake sijui kamwambiaje... mi najionea kero tu!
 
Back
Top Bottom